Niliacha Umalaya Baada ya Kujikuta Guest Nikiwa na Baba Yangu Mzazi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Joy Ndirangu alijipata katika hali ambayo kamwe hakuna anayewahi kutamani kujipata .

Mwanadada huyu mwenye umri wa miaka 32 amekuwa akifanya kazi ya ukahaba kwa miaka 9 , tangu alipomaliza shule ya upili . Anasema haikuwa kupenda kwake kujiiingiza katika kazi ya kuuza mwili wake lakini hali ya umaskini ,mateso ya kukosekana kwa kazi ndio baadhi ya sababi zilizomsukuma hadi akajipata katika biashara ya ukahaba hapa Nairobi .

Alipomaliza shule ya upili , Joy alikuja Nairobi kutafuta kazi kwa sababu wazazi wake huko Subukia ,Nakuru hawakuwa na pesa wala mipango ya kumpeleka katika chuo chochote kwa mafunzo zaidi .

Akija Nairobi ,alikuwa mwingi wa matumaini kwamba angepata kazi ili arudi shule mwenyewe .Alianza kuishi na jamaa yake mmoja maybe pia alikuwa mtu kutoka kwao Subukia .

Bila kujua kazi ya huyo ‘shangazi’ yake ,Joy alijipata katika shimo ambalo hangeweza kujitoa .Jamaa yake huyo ambaye alimwita shangazi ingawaje uhusiano wao wa kifamilia ulikuwa wa mbali alikuwa ‘madam’ –jina linaloitwa wanawake ambao huwaingiza wasichana katika ukahaba na kasha kuchukua kiasi cha fedha wanazolipwa wasichana hao katika kazi ya kujiuza.

Alishangaa ni vipi shangazi yake alimudu kuishi katika nyumba nzuri nay a gharam ya juu mtaani Highrise ingawa hakuwa na kazi maalum iliyojulikana .

Kumbe alikuwa anampa tu Joy muda wa kuzoa jiji kabla ya kumwingiza kaika ukahaba Baada ya miezi miwili ,shangazi yake alimkalisha chini na kumuambia yote! Joy alishangaa atafanya nini lakini hakuwa na chaguo jingine ila kukubali kufanya ukahaba -na hapo safari yake katika biashara hiyo ya aibu ikaanza .
Alijidanganya kila mara kwamba ataifanya muda tu kasha aiache na ajishughulishe na kitu kingine lakini anasema ukahaba ni kama uraibu .Wakati fulani hutaki kuacha kabisa kwa sababu ya mazoea na pia unapata uzoefu na wateka ambao pesa zao unazipata kama ada .

Lakini kwa Joy mgutuko ulimjia siku moja akiwa katika danguro alikokuwa akipiga shughuli yake akamwona mwanamme aliyevalia koti na mwenye umri wa juu kidogo akiingia katika sehemu ile .

Kwa sababu ya giza na alivyokuwa mbali hakuweza hasa kumjua kwa urahisi na kama kawaida yao,wanawake wote ambao walikuwa nje ya lango walimkimbilia mzee Yule ili awachague wampe raha ya mwili usiku huo .

Mzee alikuwa amevalia kofia iliyofunika sehemu kubwa ya uso wake na hivyo haikuwa rahisi kumtambua .Walipomfikia ,Joy alikuwa wa kwanza na mzee akamchagua yeye kama ambaye wataingia naye danguroni kwa shughuli ya kufurahisha nyama za ‘kimwili’.

Ole wake ! walipofika katika cha ghorofa ya juu ,mzee aliitoa kofia yake na miwani .Joy alikuwa mbele yake na hivyo alianza kwa kutoa nguo yake ya juu kabla ya kuwasha taa.kulikuwa na mwanga kutoka dirishani lakini Mzee alipowasha taa ya chumba hicho ndipo ulimwengu wake ukatikisika .

Joy alionana macho kwa macho na babake mzazi .Muda wote wakiingia katika chumba kile mzee hakusema neon na abaada ya kumchagua Joy walianza kupandaa juu .

Maskini mzee alipoangaliwa kwa makini akagundua kwamba Yule kahaba aliyetaka kula uroda naye usiku ule alikuwa binti yake! Joy hakungoja kuitwa na babake ,alianza kutoka nje ya chumba kile akilia.Mzee hakusema lolote naye akaketi kitandani akizungumza lugha ya nyumbani pekee pale . Alivyoondoka pale ,Joy alikata kauli ya kutorejea kufanya tena kazi ya ukahaba . Baba na bintiye hawakuzungumziana kwa miaka takriban mitano iliyofuata na hakuna aliyesema jambo lolote kuhusu tukio hilo .

Photo Credits: Radio Jambo
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad