2/13/2020

Ommy Dimpoz apata mwaliko kushuhudia mchezo wa NBA ALL STAR nchini Marekani, Hawa ndio mastaa watatu tu kutoka Afrika walioalikwa


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Omary Nyembo Ommy Dimpoz ni miongoni mwa mastaa watatu wa Afrika ambao wamepewa mwaliko rasmi wa kuhudhuria michezo ya NBA All-Star ambayo itafanyika mjini Chicago Marekani kuanzia February 14 hadi 16 mwaka huu.

Dimpoz ambaye ameutaja mwaliko huu kama bora na mkubwa kwa mwaka huu, ataungana na Sho Madjozi wa Afrika Kusini na Jidenna wa Nigeria & Marekani.

Mwaliko huu ni kutoka Chama cha Mpira wa Kikapu nchini Marekani – NBA, kupitia NBA Africa ambao wamemgharamia kila kitu ikiwemo Usafiri wa ndege kwenda Marekani, Usafiri wa ndani na gharama za kuishi akiwa pamoja na meneja wake (Seven Mosha) katika tukio hilo kubwa la mwaka.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger