2/14/2020

Siwezi Kumsamehe Mke Wangu, Ametembea na Mkurugenzi wa Ofisini Kwake

Baada ya kupoteza kazi yangu niliyumba sana, niliwaza nitaishije bila kazi hapa mjini, hata hivyo nilijipa moyo kwamba kwa kuwa wife ana kazi Basi mambo madogo madogo hayatasumbua wakati huo nami nitakua nakazana kutafuta kazi nyingine.

Kumbe nilikua nimekosea kuwaza hivyo, ilianza taratibu kama mzaha wife kuchelewa kurudi na kuja kuanzia saa tano usiku na kuendelea kwamba wamelazimika kufanya overtime.

Baada ya wiki kadhaa visingizio vikaisha akawa hana cha kusingizia tena, anakuja usiku ule ule mwingi bila kunisemesha chochote na kupitiliza chumbani kulala moja kwa moja bila kula wala kuoga.

Nikajiuliza, kwa biologia ya wanawake ilivyo na joto la Dar inawezekana wife akarudi na kulala tu bila kuoga? Na chakula je ina maana analala na njaa? Nikasema nitapata tu majibu ya maswali Haya, only time will tell.

Hadi napoteza kazi yangu sikua namiliki Gari wala wife hakua nalo, baada ya hizi harakati za kurudi usiku mwingi na kutoshinda home weekend nzima hatimaye wife """"" akanunua Gari""""" Toyota IST.

Nilikua naumia rohoni kwa suspicion but sikujua where and how to start investigation on that particular matter hadi siku moja tulienda pamoja na wife kwenye Gari lake na mdogo wake wa kike aliyekuja toka Jana yake.

Mimi niliomba nikae nyuma wao mbele, kabla hatujaondoka nashangaa kuiona chupi ya wife bikini pembeni ya miguu yangu ndani ya Gari, kwa kifupi ile safari ilikufa.

Nilimtoa ndani ya Gari kwa kipigo kikali sana nikitaka kujua kulikoni hiyo chupi kuwepo humo, hakawa hana cha kujitetea, nikamfungua chumbani na nikachukua simu zake zote nikawa nazo sebuleni, tangu kufunga ndoa sikuwahi kumpiga zaidi ya siku hiyo.

Hapo sebuleni nilipitia meseji zote kwenye simu zake, baada ya zoezi hilo nililidhika beyond reasonable doubt my wife was seeing someone else.

Na mtu huyo alikua ni mkurugenzi wake kazini, na hiyo kampuni anayofanya wife ni ya huyo bosi, nikamfungulia saa tatu usiku na kumpa simu zake nikaendelea na mambo mengine.

Sikupata usingizi siku hiyo, nilikaa kwenye TV nikibadilisha Chanel mbali mbali, saa nane usiku alinifuata sebuleni na kupiga magoti akaniomba msamaha kwa machozi kwamba hatorudia, haelewi kwa nini alifanya vile, sikumjibu nikamwambia arudi alale.

Nika conclude kwamba sina mke, nikaazimia kwamba nisilete fujo, kwa hali niliyonayo nijifanye ---- tu huku moyoni nikijua sina mke, halaf niendelee ku fight nikifanikiwa niachane nae niendelee na maisha yangu.

Wife ali pretend kwamba ametubu na ameachana na yule jamaa, lakini kwa siri aliendelea nae, hakujua kama mimi najua yule mpenzi wake ndie bosi wake kazini, alikua amenidanganya kwamba ni mteja wa kampuni yao na kwamba hawaonani tena.

Kunipumbaza, kwa mara ya kwanza, ilikua ni Ijumaa, akaja na bahasha akanipa ilikua na million mbili za elfu kumi kumi, kaniambia amepata kazini baada ya kufanya deal, nikazipokea nikaziweka benki, Ili kuni fool kila siku mbili tatu au wiki alikua ananiletea pesa, laki tano na kuendelea nami nikawa natunza pesa nikikusanya mtaji.

Nikaanza kufanya shughuli zangu za kibiashara, kidogo kidogo mambo yangu yamekua mazuri kwa pesa hizo hizo za uzinzi wa wife, yeye kwa kipindi chote anaamini kwamba amenifanya ----, akienda kulala kwa hotels na huyo jama, wakati mwingine akiaga anakwenda safari kikazi kumbe yupo humu humu Dar, nami nikajifanya mjinga nikajiimarisha.

Kila jambo lina mwanzo na mwisho, mkurugenzi kapata msichana mpya kazini inaonekana mke wangu katemwa, yupo tu nyumbani namuacha hapo asubuhi naenda kwa business zangu narudi jioni, nikimuuliza kulikoni analia tu, yupo frustrated, ndipo nikapata chanzo kikanieleza yaliyotokea huko kazini kwao, mapenzi na bosi yamefikia mwisho.

Nimeishi kwa mateso rohoni kwa miaka 4, huku nikificha hasira yangu, nikishiriki tendo la ndoa, ili kumhadaa huyu mzinzi bila yeye kujua, sikuwahi kupata wazo la kufumania kwa kua nilikua nitaharibu mpango wangu.

Wiki hii najiandaa kuhamia kwangu ingawa ni vyumba viwili na sitting room but it is my home, naenda kuanza upya
Nasamehe mtoto pia, nitapata mwingine, kwanza sina imani kama ni wangu, nitaondoka na begi tu.

Yote Tisa, kumi nimepona rohoni, nasikia amani sana.

Kusamehe ni msamiati kwangu kwa sasa, hatua hii niliipanga miaka minne nyuma.

Ama kweli poteza kazi ndo utajua sura halisi ya mkeo

  By Jean pierre oberoi
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

11 comments:

 1. Duuuuuu ni mwanamke niliyesoma hiii habari lakini natamani kulia

  ReplyDelete
 2. Hapo kulikua hakuna penzi la dhati baina ya wote wawili, story tu mepata kwa upande mmoja upande mwingine hatujui kilicho msibu mpaka akaamua kuchepuka, Ndoa ni ngumu pale wana ndoa mnapoingia kwa malengo, sio kwa upendo wewe kama umeamua kwenda nenda ila mtoto ni malaika hana kosa kama unahisi sio wako kapime DNA lakini kumtelekeza sio sahihi, who knows labda mbegu unayo hiyo moja unategemea jila ukikojoa ni mbegu yenye mtoto,,,, shauri yako samehe saba mara sabini.

  ReplyDelete
 3. Wanawake wote kwa ujumla ndivyo walivyo. Hasa hiki kizazi cha sasa hivi huwezi kuwaamini sana.

  ReplyDelete
 4. Duuh! Ni kweli kabisa, yeye ushamtia adabu, lakini mtoto wako usimtekeleze. Hata kama hutamchukua, mtunze ni wako tu! Isitoshe wazimu aliuanza baada ya wewe kukosa kazi, yamkini mwanzo alikuwa mtulivu tu. Pole sana, usiombe kuvulugwa katika mapenzi, ni mtihani mkubwa.

  ReplyDelete
 5. pole kaka kama ingekua wewe ndo umefanyiwa hivyo ungejisikiaje? maisha ya ndoa ni magumu sana ndo maana kuna kusemehe, ipo siku na wewe unaweza kusaliti ndo yako kama yeye arafu utasemaje? kumbuka kila mtu anamapungufu yake unaweza kwenda kwa mwingine akawa anatabia mbaya kuliko hata huyo.

  ReplyDelete
 6. ovyo kabisa wewe mwanaume,sasa mtoto ana kosa gani?hata wewe hukua na mapenzi na mkeo na kwa upuuzi huo ni wazi wewe ndo chanzo cha mkeo kuchepuka. unaonekan huna busara hata robo upo kimaslahi tu. kama humtaki mbona hela zake zimekufanya uwe ulivyo na kuja kuandika huu utobo wako humu ukiwa full confidence? mbona yeye hakuhama nyumbani ulipokuwa huna kazi? peleka upumbavu wako huko kwanza hutopata hyo amani unayoitarajia

  ReplyDelete
 7. msamehe tu kumbuka unafanyabiashara kwa uzinzi wake yeye huenda alifanya kwsabu hukuwa na kazi na majukumu yalikuwa mengi...kaa utulizane na mkeo mlee mtoto-bila ya hasira yyt-kwani bila ya yeye kwa sasa ungekuwa unapakatwa tu..man think positive no negative..ndo maana uko poa sasa hivi jasho lake hilo la sivyo-litakurudia nyuma wewe,..kama hasingekupenda pesa angepeleka kwao au anapopajua yeye....

  ReplyDelete
 8. Kha! Kweli mwanamke kakosea, Ila me nashanga unavojiona umewin Wakati mafanikio yako nikutokana na hela aliyohingwa mkeo. Kwa maana nyingine huyo bosi kakuwezesha na wewe nayo mafanikio. Pili kukataa mtoto kunakuonyesha ulivo limbukeni

  ReplyDelete
 9. Tatizo ni kwamba mwanamke akichepuka ndio malaya, ila mwanaume ni haki yake! huyo mkeo anaonekana wazi anakupenda ndio maana alikupa hata hizo hela. Alafu kitu kingine wewe unaonekana humpendi mkeo, ungekuwa unampenda ungemsamehe maisha yaendelee. Wanaume bwana "always perfect"

  ReplyDelete
 10. Hela yake sio haramu? Tamu kama asali ila yeye ndo mbaya? Si ungeondoka baada ya kujua? Yaani umemtumia mtoto wa watu kupata mtaji afu usepe?ovyoooo tena itakuwa ushapata mwingine wewe

  ReplyDelete

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger