Wanajeshi 10 wa Tanzania wapoteza maisha wakati wakifanya mazoezi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Jeshi la Ulinzi la Tanzania limetangaza kuwa askari 10 wa jeshi hilo wamepoteza maisha wakati wakifanya mazoezi.

Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya nchi hiyo (CDF), Jenerali Venance Mabeyo ambapo ameongeza kuwa sampuli za wanajeshi hao waliopoteza maisha katika mazoezi ya kijeshi zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali  kwa ajili ya uchunguzi.

Mabeyo ameyasema hayo jana katika ikulu ya Dar es Salaam baada ya Rais John Pombe Magufuli kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hapo Januari 31, 2020.

Kwa mujibu wa Mabeyo, wanajeshi hao walikuwa kwenye mazoezi ya kawaida ya kutembea. Ameendelea kubainisha kuwa baada ya saa mbili hali zao kuanza kubadilika wakiwa eneo la Msata, walipelekwa hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya nchi hiyo (CDF), Jenerali Venance Mabeyo ameendelea kufafanua kuwa baada ya kulazwa hospitalini hapo, baadhi yao walifariki dunia na wengine hali zao ziliimarika na kwamba hadi sasa kuna majeruhi watano.

Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais Magufuli alitoa pole kutokana na vifo vya watu 20 katika kongamano la mhubiri wa Kikristo, Boniface Mwamposa vilivyotokea mjini Moshi, vifo vya watu 21 mkoani Lindi baada ya nyumba zao kusombwa na maji na vifo vya wanajeshi hao 10.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad