3/20/2020

Corona yakwamisha kina Ester kupatiwa matibabu nje

 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kinaangalia namna ambayo itawawezesha kuwasafirisha Wabunge Ester Bulaya, Halima Mdee na Jesca Kishoa kwa ajili ya kupatiwa matibabu nje ya nchi kwa kuwa hali zao bado hazijatengemaa.


Akizungumza leo Machi 19, 2020, na EATV&EA Radio Digital, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mrema amesema kuwa kulingana na hali ya maambukizi ya Virusi vya Corona ilivyo kwa sasa inawawia vigumu kuchukua maamuzi yoyote, kwakuwa nchi walizodhamiria kuwapeleka tayari zimekwishakumbwa na visa vya ugonjwa huo.

"Kina Ester wameruhusiwa juzi, isingekuwa Corona tulikuwa tunafikiria kuwapeleka nje kupata matibabu zaidi, lakini bado tunawaza nini cha kufanya, hali zao bado hazijatengemaa, hasa Ester aliyeumia ndani huwezi jua nini haswa kinasumbua, tulitaka kuwapeleka kwenye nchi ambazo zina matibabu mazuri kuliko sisi kama Kenya na Afrika Kusini" amesema Mrema.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

1 comment:

 1. Kweli nyie no matapeli.
  Mmenifanya mimi nichangie pesa yangu ya Boda Boda kwa kudhani/Kuamini kuwa Ruzuku imeliwa na mnya Kiti.

  Kumbe mna hela ya kwenda kupandia ndege mpaka sauzi. Hela ya tabibu pia Atataka Randi Landa elfu kumi mnazitoa wapi. Kama Si wadanganyifu tuwaitaje?

  Betrayers of trust or Victimized Drama..??

  AU MNAFIKIRI NA SISI NI BUNGENI MFANYE USANII MPAKA MNAKOKOTWA NJE.

  HAPA A PESA YANGU NAITAKA KULISHA WANANGU.

  NA Wazazi WA Malehemu Akwilina na Jamuhuri wakikata Rufaa mtakuja kutuomba sisi Tena?

  Nataka Jibu...!!! Swindlers

  ReplyDelete

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger