DC Sabaya Awashukia Madaktari wa Twitter, Instagram na Facebook Kuhusu Ugonjwa wa Corona

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, amepiga marufuku watu wanaojifanya kuwa ni madaktari na kuanza kutoa ushauri kupitia mitandao ya kijamii, kwani kwa kufanya hivyo inazidi kuleta taharuki na mkanganyiko kwa Watanzania.

Sabaya ameongeza kuwa kipindi hiki ambacho Dunia inahangaika kukabiliana na ugonjwa hatari unaosababishwa na Virusi vya Corona ni vyema suala la utolewaji wa elimu likafanywa na wataalamu wa afya pekee.

"Madaktari wa Twitter, Instagram na Facebook tunawaomba katika hili muwapishe wataalam na Madaktari wa Binadamu wafanye wajibu wao!, mnachochangia zaidi katika hili ni confusion(mkanganyiko)!, suala hili linahusu maisha ya watu na sio siasa za bei rahisi" amesema DC Sabaya.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jitto mrumia Mada. Mjuzi WA yote. Kaa huko huko kwenu twita.

    Waache Wana taaluma watujuze na siyo Kilaza wewe.

    ReplyDelete

Top Post Ad