3/31/2020

Hatuwezi Tuka 'Copy' na Kupest Kwa Wazungu - Spika Ndugai


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema kuwa kama nchi haiwezi kuchukua tahadhari kama zilivyochukuliwa na Mataifa mengine duniani ya kupambana na Virusi vya Corona kwa kuwa watu wengi nchini maisha yao ni ya kubangaiza siku kwa siku.

Hayo ameyabainisha leo Machi 31, 2020, Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 Mkutano wa 19.

"Hatuwezi kuchukua measure za wazungu na kuzi copy na ku- paste hapa kwetu kama zilivyo, tutaua watu wetu, lazima tuangalie maisha yetu ya Kitanzania na kujaribu kuchukua hatua kufuatana na mazingira yetu" amesema Spika Ndugai.

Aidha wakichangia hoja zao bungeni wabunge wa CHADEMA Halima Mdee na Peter Msigwa, wameishauri Serikali kuja na taarifa zote zinazohusu mwenendo wa ugonjwa wa Virusi vya Corona hapa nchini na kuangalia ni kwa namna gani kwa pamoja wataweza kukabiliana na athari ikiwemo uchumi pindi ugonjwa huo utakaposambaa zaidi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

1 comment:

 1. Mzee wa Twita wa kukopi na kupest.
  Umesha pata Jibu lako toka kwa Mshua.!!

  Tutafanya yetu kwa Mujibu wa Mazingira
  yetu na Hali Halisi ya Mtanzani.

  Umesikia Mzamiaji.??? Juni inakalibia.

  ReplyDelete

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger