3/27/2020

Mbowe na Familia yake Wabainika Hawana Corona Wakiwa Karantini Baada ya Mtoto KunaswaFamilia ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe imesema baada ya mtoto wao kukutwa na ugonjwa wa Corona familia nzima ilijikarantini ili kupunguza uwezekano wa kuwaambukiza wengine.

Ujumbe mfupi uliotolewa na Mbowe ikiwa ni siku kadhaa tangu mtoto wake kukutwa na ugonjwa huo umeeleza kuw wanafamilia wengine ni wazima wako salama na hawana ugonjwa huo.

“Baada ya Mwanangu Dudley kuwa positive na virusi vya Corona, familia nzima (Dar na Dodoma) iliingia kwenye “self isolation” kuondoa uwezekano wa kuambukiza wengine endapo tungekuwa na sisi tumeambukizwa”

Poleni wote kwa hofu na asanteni sana wote kwa sala zenu! Indeed, ours, is an Amazing and Loving God.

“Hata hivyo tutaendelea kuwa kwenye isolation hadi siku 14 zinazoshauriwa zitimie kamili, Nawasihi wote tuendelee kuchukua tahadhari zote kwa kadiri na ushauri unaotolewa, Mbarikiwe sana”
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger