3/26/2020

Mwenye Nyumba Awasamehe Kodi Wapangaji Kisa CoronaBABA mwenye nyumba mmoja kutoka Nyandarau nchini Kenya amewasamehe wapangaji wake kodi ya nyumba ya miezi miwili ili watumie pesa hizo kujiandaa dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Amefanya hivyo ili kuwapa nafuu wapangaji wake katika kipindi hiki ambacho kazi na biashara hazifanyiki kutokana na kuepuka kusambaa kwa corona.

Ameongeza  kuwa anajua corona itaathiri watu wote wakiwemo wafanyakazi ambao wengine wao wanaishi kwenye nyumba zake, hivyo inawapasa washirikiane serikali katika mapambano hayo.

Hadi sasa Kenya imeripoti visa vya wagonjwa 28 wenye virusi vya corona huku mgonjwa wa kwanza kukutwa na virusi hivyo tayari akiwa amepona.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger