3/24/2020

Paul Makonda Atoa Kali "Mtoto wa Mbowe Anaugua CORONA Ndio Maana Amesitisha Mikutano ya Chadema"

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amewataka wananchi kusikiliza kauli za Serikali juu ya namna gani watajikinga na kupata maambukizi ya Virusi vya Corona na waachane na wanasiasa kama kina Mbowe kwa sababu wao wanangoja ndugu zao waugue na wao ndio wasitishe mikutano yao.

Makonda ameyabainisha hayo leo Machi 24, 2020, wakati wa ziara yake maalum katika stendi ya Mabasi yaendayo mkoani ya Ubungo.

"Tusikubali kupokea ushauri na ushawishi wa wanasiasa uchwara kama kina Mbowe kwa sababu asingeugua mtu wa familia yake aliyetoka nje akaja na huo ugonjwa mngeingizwa kwenye mikutano na kuleta mvutano na Dunia ingeona Tanzania haina demokrasia, mkiacha kuwasikiliza watalamu wa afya na kuwasikiliza waganga wa kienyeji na washirikina kama kina Zitto Kabwe kazi kwako" amesema Makonda.

Jana Machi 23, 2020, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, alitangaza kusitisha kufanya mikutano yake ya hadhara nchi nzima, ambayo alitangaza kuianza Aprili 4.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

4 comments:

 1. huyu si alisema siri ya mgonjwa isitolewe na mtu yoyote bila doctor, sasa yeye anafanya nn.

  ReplyDelete
 2. Jitoo Kambwe ,mzee waTwita na fezibuku
  amekuwa mpiga hitekenoloji ya stimulasi
  pekegi . mtaalamu wa Fm Sw na flikwensi
  zote.

  ReplyDelete
 3. Mh. Makonda Korona ni tauni, tunajinyenyekeza mbele za Mwenyezi Mungu na kumuomba asamehe dhambi za kila mtanzania na makosa yaliyotendwa kwa namna moja au nyingine na mamlaka zozote ziliziwahi kuwa nchini including taasisi za kidini nk. Hii ni kwetu wote, kipindi hiki kiwe cha unyemyekevu ili Bwana aliponye taifa 2 Nyakati 7 :13-14. Upendo au kupendana na kusameheana ni muhimu. Hatufurahi yeyote kuumwa korona hata kama aliwahi kukosa huko myuma. Kipindi hiki ni cha toba

  ReplyDelete
  Replies
  1. Uungwa na Utu wa Mbunifu mchapa Kazi kijana wetu Makonda ameweza kuwaombea na kusisitiza kwa ku waagiza matabibu na wauguzi kumtibia na anafatilia kwa karibu maendeleo ya wana classic baby na kijana wa basata na mwanafamilia wa mnyakiti wa upande wa Kumchuzi.ameamua kusitisha mikutano kwa ajili hiyo. hivyo ni raia wa wapi?

   Delete

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger