Raia 13 wa China wazuiwa kuingia Kenya wakitokea Tanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Kenya. Watu 16 walizuiwa kuingia nchini Kenya kupitia mpaka wa Lunga Lunga katika mji wa Kwale wakitokea  Tanzania
Kati ya watu hao, 13 ni raia wa China.


Raia hao wa China ni Xiao Zhanquan, Xu Shaul, Xu Duo, Lyu Xiaohua, Zhou Changyong, Jiang Chunyang, Xiao Zhanquan, Lyu Xiaohua, Wang Xiaoba, Shang Deyuan, Huang Honghui, Yang Yubiao na Cao Bingwang.

Watu hao walisindikizwa na madereva watatu wa Tanzania ambao ni  Saidi Seif Mapunda, Hassan Mohammed Makolo na Wema Ramadhani Muambeya.

Ripoti ya Polisi iliyoonwa na kituo cha runinga cha Citizen Kenya inaonyesha watu hao waliwaambia wakaguzi katika eneo hilo kuwa  walikuwa wanaelekea mjini Mombasa kwa ajili ya kazi maalumu katika kampuni ya Bamburi Cement Ltd.


Hata hivyo, baada ya mahojiano zaidi ilitakambulika kuwa tangu  walipowasili nchini Tanzania kati ya Machi 4- 16, 2020 hawakutimiza siku 14 za kujitenga katika karantini zilizowekwa kwa ajili ya kujikinga na virusi vya corona.


Wote 16 walizuiwa  kuingia Kenya kutokana na kutokidhi maagizo ya kujikinga na kuzuia kuenea kwa virusi vya corona na walirudishwa mpakani.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad