3/31/2020

Rais wa Brazil Apuuza Ugonjwa wa Corona " Ni Mafua tu Kwanza Ipo Siku Wote Tutakufa"Rais Jair Bolsonaro amevifananisha virusi vya #Covid19 na ‘Mafua’ na kuwataka raia kuendelea na ujenzi wa uchumi na kusema sababu ya kutowazuia raia kutoka nje ni kuwa wote kuna siku watakufa

Wizara ya Afya ya Brazil imeripoti visa 3,904 vya maambukizi ya #Covid19 na vifo 114 ambapo Bolsonaro aliwaambia wafuasi wake "Virusi viko, itabidi tukabiliane navyo. Tuvikabili kama wanaume, sio mvulana"

Pia amevishutumu vyombo vya habari vya nchi hiyo kwa kukuza sana kuenea kwa virusi hivyo na kusema wanaeneza hisia za woga, kwa kutumia wanaokufa nchini Italia ili kuleta wasiwasi

Rais aliuliza wiki iliyopita kwanini shule zifungwe ikiwa ni watu wa zaidi ya miaka 60 ndiyo walio kwenye hatari ya kuambukizwa na virusi hivyo?
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger