3/31/2020

Rwanda Kinara idadi ya Waathirika wa Corona Afrika Mashariki


Rwanda inaongoza kwa visa vya maambukizi ya ugonjwa wa corona katika kanda ya Afrika Mashariki ikiiwa na wagonjwa 70, ikifuatiwa na Kenya 42, Uganda 33, Tanzania 14, huku Burundi na Sudan Kusini zikiwa hazijarekodi visa vyovyote vya maambukizi.

Katika hotuba yake kwa taifa usiku wa Ijumaa Rais Paul Kagame alisema idadi hiyo ya maambukizi ya virusi vya Corona itaendelea kuongezeka kwasababu wale waliokutana na waathirika wanaendelea kutafutwa ambapo amesema serikali inatoa msaada wa chakula kwa familia zisizojiweza na ambazo zimeathiriwa na amri ya kukaa nyumbani.

Waziri wa afya wa Rwanda alikiambia kituo cha televisheni cha Rwanda kwamba hali hiyo ya maambukizi ilitokea baada ya wafanyibishara wengi wa Rwanda kurejea nyumbani kutoka Dubai, serikali ilipotangaza kuwa itafunga mipaka yote ya nchi.

Ambapo mpaka hivi sasa Rwanda inajumla ya wagonjwa 70 wa corona, 32 kati ya hao waliwasili nchini humo kutoka Dubai.

Hata hivyo katika visa vya hivi karibuni vya maambukizi, watu sita walitokea Dubai, wawili kutoka Afrika Kusini, mmoja kutoka Nigeria na mwigine alikuwa amesafiri maeneo ya Afrika mashariki hivi karibunii, ilisema taarifa ya wizara ya afya nchini humo.

Mwanzoni mwa juma lililopita, Rwanda ilitangaza kufunga mipaka yote ya nchi hiyo na watu kuamrishwa kusalia majumbani mwao katika juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Hata hivyo  watumishi wote wa serikali na wa kibinafsi  wametakiwa kufanyia kazi nyumbani na safari za kuenda mikoani kusitishwa kwa wiki mbili kukiwa na uwezekano wa muda huo kuongezwa ambapo vilabu vya pombe na, maduka yasio ya chakula pia yamefungwa huku usafiri wa bodabobda ukisitishwa.

Hatua hiyo ilichukuliwa siku moja baada ya wizara ya afya ya Rwanda siku ya Jumamosi kutangaza kuwa watu wengine sita wameambukizwa virusi vya corona miongoni mwao mtoto mchanga wa miezi 10.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger