Afariki kwa Kupigwa Radi Akiwa Anatokea Shambani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mkazi wa kata ya Kabungu mkoani Katavi, Paulo Chundu (27) amefariki dunia kwa ya kupigwa na radi wakati akitoka shambani.

Tukio hilo lilitokea machi 29 mwaka huu majira ya saa 12: 45 jioni katika mbuga za kalilankulukulu kata ya kabungu wilayani Tanganyika mkoani katavi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoni katavi Benjamin Kuzaga amesema kijana huyo alikutwa na umauti akiwa katika mbuga hiyo akiendesha pikipiki kutokea katika Kijiji cha ikaka akielekea nyumbani kwake.

Kamanda alisema majira ya saa 12:45 alipatiwa taarifa za kijana huyo kufariki kwa kupigwa radi akiwa anatokea shambani kuelekea nyumbani

Baba mdogo wa kijana huyo, John Laurent alisema alimuagiza shambani kumpeka mtu wa kufanya kazi za shambani ikiwemo kutoa majani, hivyo wakati anarudi akafariki kwa kupigwa na radi.

Alisema tukio hilo limemuumiza na kwamba mtoto huyo aliachiwa na kaka yake baada ya kufariki na kupewa jukumu la kumlea.

Magreti maiko mama mdogo wa marehemu alisema siku hiyo hawakupata taarifa yoyote juu ya kifo chake ila walikuwa wakishangaa kwanini hajarudi nyumbani hadi usiku na taarifa walizipata siku ya pili wakiambiwa kuwa kunamtu amepata ajali ya pikipiki.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad