google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Ujangili wa wanayamapori wadogo kwa kivuli cha kitoweo kukomeshwa | UDAKU SPECIAL

Ujangili wa wanayamapori wadogo kwa kivuli cha kitoweo kukomeshwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amekiagiza Kikosi Dhidi ya Ujangili ( KDU)  Kanda ya Kaskazini kuongeza mbinu katika kukabiliana  na ujangili wa wanyamapori wadogo wadogo wanaouawa kwa ajili ya kitoweo na baadhi ya wananchi wanaoishi  maeneo yaliyo karibu na Hifadhi.

Ametoa agizo  hilo leo  mkoani Arusha  wakati alipokuwa akizungumza na Watumishi wa kikosi hicho kinachokabiliana na na ujangili katika mikoa ya Arusha, Tanga, Kilimanjaro na Manyara.

Hatua hiyo inakuja kufuatia nguvu kubwa na mashirika ya Kiuhifadhi ya ndani na nje ya nchi kujielekeza  katika ulinzi wa wanyamapori wakubwa kama vile tembo, faru, twiga, simba pamoja chui huku wanyamapori wadogo wakiwindwa kwa kasi na jamii zinazopakana na hifadhi kwa ajili ya kitoweo.

 Akizungumza katika mkutano huo, Kanyasu amesema endapo hatua za makusudi hazitachukuliwa kukabiliana na tatizo hilo jamii nzima itakuwa hatarini wanyamapori kama vile  Simba wataanza kuwala binadamu kwa vile wanyama wanaotegemewa kama chakula chao watakuwa wamekwisha kwa ujangili.

Amewataja wanyamapori hao wadogo wanaowindwa  ni kama vile  swala, pundamilia, sungura, nguruwepori  pamoja  na digidigi

Mbali ya athari hiyo, ametaja athari zingine ikwemo wanyamapori wakubwa watatoweka kwa kukosa chakula na hivyo sekta ya utalii itaathirika kwa vile kutakuwa na hifadhi zisizo na wanyamapori.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad