3/25/2020

Wanajeshi 92 Wauawa na BOKO Haram....


Rais wa Chad, Idriss Deby amesema Wanajeshi 92 wa nchi hiyo wameuawa katika shambulio lililofanywa na Boko Haram katika eneo la Boma na kudumu kwa takriban saa 7

Ametaja shambulio hilo kuwa baya zaidi kutokea nchini humo na kwamba hiyo ni mara ya kwanza kwa Chad kupoteza Wanajeshi wengi ndani ya siku moja

Imeelezwa kuwa vikosi vilivyotumwa kusaidia Jeshi navyo vilishambuliwa na Boko Haram, ambao walifanikiwa kuchukua silaha za Jeshi. Aidha, magari 24 ya kijeshi pia yameharibiwa vibaya katika shambulio hilo

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN), mashambulizi ambayo yamefanywa na Boko Haram kwa muda wa miaka 10 yamegharimu maisha ya watu 36,000 na kusababisha wengine Milioni mbili kukimbia makazi yao
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger