3/20/2020

Wema: Siwezi Kukaa na Kinyongo Watu Wengi Wananikosea SanaBIBIE Wema Sepetu amesema kuwa katika vitu ambavyo hawezi kuishi navyo moyoni ni kinyongo, kwa sababu anaamini kukaa na kinyongo ni sawa na kujizibia riziki na kuzuia mambo yako yasiende.

Mrembo huyo anafanya poa kunako anga la sinema Bongo, amesema kuwa, ukiona amemchukia kweli mtu, basi ujue kuna kitu kikubwa kamfanyia, lakini mbali na hapo, yeye ni mtu wa kusahau na kusamehe kisha kuacha maisha yaendelee.

“Watu wengi sana wananikosea, lakini ukweli ni kwamba siwezi kukaa na kinyongo kwa muda mrefu moyoni mwangu, mimi huwa nasahau na kusamehe pia kisha mwisho wa siku namuachia Mungu ndio anadili na wabaya wangu,” alisema Wema.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger