5/28/2020

Baba Amkatakata na Kumuua Mwanawe wa Kike Kisa Kufunga ndoa Kisiri IranMaafisa wa polisi nchini Iran wamemkamata mwanamume mmoja anayetuhumiwa kumuua mwanawe wa kike mwenye umri wa miaka 14 katika kile kinachotajwa kuwa 'mauaji ya heshima' ambayo yamezua hisia kali na ghadhabu.

Romina Ashraf alitoroka nyumbani kwao katika mkoa wa Gilan na mpenzi wake mwenye umri wa miaka 35 baada ya babake kupinga waowane, vilisema vyombo vya habari vya eneo hilo.

Wawili hao walikamatwa na maafisa wa polisi kabla ya Romina kurudishwa nyumbani licha ya kuwaambia maafisa hao kwamba alikuwa anahofia maisha yake.

Alhamisi iliopita , anadaiwa kushambuliwa na babake katika chumba chake.

Chombo cha habari cha Gilkhabar.ir kiliripoti kwamba Romina alikatwakatwa na baadaye babake akatoka nje na kifaa alichokitumia kufanya kitendo hicho na kukiri kumuua.

Siku ya Jumatano, baadhi ya magazeti yaliangazia tukio hilo katika ukurasa wao wa kwanza.

"Nyumba ya baba isio salama", kilisema kichwa cha habari cha gazeti linalounga mkono mabadiliko Ebtekar, ambalo lilizungumzia kuhusu ukosefu wa sheria zilizopo kuwalinda wanawake na wasichana.

Wakati huohuo, Hashtag ya #Romina_Ashrafi imetumika zaidi ya mara 50,000 katika mtandao wa Twitter, huku watumizi wake wengi wakilaani mauaji hayo na kuhoji sheria zinazowalinda wanawake kwa jumla
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger