5/27/2020

Mwanamuziki Burna Boy Aripotiwa Kukamatwa na POLISI Baada ya Majirani zake Kuripoti Juu ya Kuzidisha Kelele

Mwanamuziki Burna Boy Aripotiwa Kukamatwa na POLISI Baada ya Majirani zake Kuripoti Juu ya Kuzidisha Kelele

Siku ya Jumapili iwe ni siku ya kupiga kelele ambazo hazijawahi kutokea. Kama una mziki mzuri nyumbani kwako, fungulia mziki kula mziki utakavyo." Inawezekana kauli hii ya Mhe. Makonda ilifika mpaka Nigeria na kupokelewa vyema na Burna Boy.

Mwimbaji huyo wa Nigeria ameripotiwa kukamatwa na polisi mara baada ya majirani zake kutoa taarifa za malalamiko kwamba msanii huyo anafungulia muziki kwa sauti ya juu kiasi cha kusababisha kelele mtaani.

Mtandao wa Pulse Nigeria umeripoti kwamba Wananchi hao wenye hasira walifika nyumbani kwa staa huyo wakiwa na polisi huku wakitoa maneno kwamba imekuwa kero kwao, huku wakimtolea mfano jirani yao mwingine mchezaji wa Man United Odion Ighalo ambaye wanasema ni mtulivu na asiye na kelele za muziki nyumbani kwake.

Kwenye video zilizonaswa na Blog ya Linda Ikeji, Jirani mwingine alisikika akisema, Burna anapiga kelele hizo za muziki nyumbani kwake wakati bado anadaiwa hela ya kiwanja alichojenga Jumba lake hilo. Baba yake mzazi ameripotiwa kukamatwa pia
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger