Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Chriss Mauki Kikaangoni....Baada ya Kuwaponda Wanaume Wasio na Hela...Wadau Mbali Mbali Wamshushua

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURENa Thadei Ole Mushi.

Hebu Leo tuongee na Hawa Motivational speeker Kuna saa hawaelewi maisha halisi watu wanayopitia. Leo ndugu yangu PhD holder Chriss Mauki kaandika kitu ambacho kwa Kweli kinakera na kuudhi. Nimeona wengi wakimjibu na Mimi Kama sehemu ya jamii niandike kitu kidogo. Chriss kaandika naomba Kunukuu...

"Ukiona umeolewa na Mume ambaye sentesi zake kutwa kucha ni "Sina hela" au "Kuna ishu flan nafuatilia ikitiki......" na Jamaa anatoka asubuhi na kurudi jioni huna haja ya kuwahangaisha mitume na manabii wakuombee. Jua tu umeolewa na Msanii."

Mwisho wa Kunukuu....haya ndio Chriss ameona awaandikie wake zetu leo asubuhi.

Hoja yangu.

Lengo la kwanza kabisa la mwanadamu kusoma na kuelimika ni kuweza ku ya mudu mazingira anayoishi kwa kupambana na changamoto za kila siku. Kama sote tunavyojuwa sio wanadamu wote wanabahatika kupata hiyo elimu, wale asilimia chache wanayopata hiyo elimu hasa elimu ya level ya PHD tunaamini kabisa hawa ni “ problem solvers” ndio watatuzi wa changamoto zote kwenye jamii watafanya tafiti watakuja na majibu na majawabu ya njia gani itatutoa hapa tulipo kwenda sehemu nyingine kama jamii.

Kaka yetu Chris Mauki yeye ana PHD tena ya psychology na zaidi ni mwalimu wa wanafunzi wetu pale chuo kikuu cha Dar. Kazi binafsi anayofanya yeye ni muelimishaji na mtoa mada za matatizo ya mauhusiano pamoja, mshehereshaji wa shuguli mbalimbali (MC) na zaidi anajipambanua kama motivational speaker (mtia watu moyo wasikate tamaa kwa kuwaonyesha njia na tumaini)

Kwa kauli yake hiyo je kwa mtu mwenye level ya PHD Kama yeye katusaidia kama jamii? Yaani nini Mchango wake kwa Hawa wanaume wanapambana na Mishe usiku na mchana?


Je hapa katatuwa changamoto ya wanaume kukosa pesa au kaongeza chumvi kwenye kidonda?

Yeye kama motivational speaker ametutia moyo wavuja jasho au katuvunja moyo?

Zaidi ya yote Chris wewe ni mchaga wachaga hatuna tabia za mipasho tena mtu wa level ya PHD sisi ni results oriented brother. Kuna watu kibao hawajasoma ni mafundi uashi, wapika supu za utumbo wachoma kongoro lakini wanapeleka chakula nyumbani kuna siku pia hawauzi mambo yanakuwa magumu na wanasema “ Kuna wateja nawasikilizia kesho mambo yatakuwa mazuri “ je hawa nao ni wasanii?

NILIDHANI KWA KUWA UPO PALE UDSM UNGEKUWA UNAJUA HAYA.

Kitu ambacho hukijui ni kuwa zaidi ya wahitimu 80,000 huhitimu elimu ya juu na katika vyuo vya Kati kila mwaka. Katika kundi kubwa kama hili kwa hali ya ajira ilivyo sasa hivi nchini ni asilimia 12 tu ya vijana hawa wenye uhakika wa kupata ajira. Zaidi ya asilimia 88 ya wahitimu Hawa huzagaa mitaani kuhangaika na maisha. Hawa wanapotoka hawajui wanarudi na Nini? Wanapotoka wanawaaga wake zao kuwa wanaenda kwenye Mishe unafikiri wangeagaje wake zao? Au kwa vile wewe umeajiriwa?

Kitu ambacho pia hukijui ni kuwa mwaka 2017 Mh Jenister Mhagama (Waziri) alisema Asilimia 71 ya watanzania hufanya kazi zisizochangia pato la taifa kabisa. Alikuwa akiwasilisha tafiti ya Taasisi ya ukusanyaji takwimu Tanzania. Maana yake asilimia 71 ya WATANZANIA ni watu wa Mishe wanaishi Kama ndege leo ipo Kesho haipo... Huwezi kuita kundi kubwa Kama hili ni wasanii.

Kitu kingine ambacho hukijui ni kuwa tarehe 12/12/2014 vijana zaidi ya elfu kumi walijitokeza kuomba nafasi 50 za kazi TRA. Unafikiri walipoondoka nyumbani walisemaje? Waliaga kuwa nawanenda kufuatilia Mishe na kwa bahati mbaya hata Mishe yenyewe haikutiki.

Si hivyo tu tarehe 13/06/2014 Vijana zaidi ya elfu 10,000 walijitokeza kuomba ajira wizara ya mambo ya ndani nafasi 70 tu. Hii ilikuwa ni kazi Migration. Si tunakumbuka wote Migration walitoa tangazo la watu 70 tu? Waliojitokeza ni maelfu ndio Hawa unaowaita wasanii leo? Maana ndani yake Kuna walioa na walikuwa wanafukuzia hii mishe na wakaikosa.

Mwaka 2016 kwenye mawasilisho ya bajeti Dr mpango alisema asilimia 90 ya wakazi wa jiji la Daresalamu hawana kazi. Hukusikia hii kauli brother Mauki? Hawa ndio unaowaita wasanii? Kisa wewe una uhakika wa Ajira na ukaendelea kulipwa? Tuache Kufuru....


Nani anaduatilia maisha ya watu waliopo sector ya Utalii kwa Sasa. Unajua maisha yao yapoje? Wanaoitwa kwenye majaribu makuu Hawa ndio tunaowaita wasanii? Maana lazima wanapotoka waage kuwa wanakwenda kwenye Mishe na wanarudi wakavu kabisa.

Chriss uungwana ni Matendo waombe msamaha Hawa wanaume. Hakika hawatakuelewa tena popote.

Ole Mushi
0712702602.

Post a Comment

0 Comments