Ticker

6/recent/ticker-posts
.

DJ Khalid "Nilirukwa na Akili SIKU Rihanna Alivyokuja na Kunigusa"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

DJ Khalid "Nilirukwa na Akili SIKU Rihanna Alivyokuja na Kunigusa"

Kila shetani na mbuyu wake, kiboko ya DJ Khaled ni mwanadada Rihanna.

Khaled amefunguka siku ambayo Rihanna alikuja na kuishika suti yake kisha kumsifia kwamba imemkaa vizuri. Anasema alirukwa na akili kusikia kauli hiyo kutoka kwa Riri

"Yo Tim, sijawahi kukwambia hii stori? Rihanna aliwahi kugusa suti yangu siku moja na aliniambia imenikaa poa, Nilichanganyikiwa." Khaled alimwambia Timbaland kwenye IG LIVE.

Hakuishia hapo, Khaled anaonekana kuyaishi maneno ya Mwana FA na AliKiba kwenye #KibokoYangu kwani aliendelea kumsifia kwa kusema kila anapoisikia sauti yake, huishiwa nguvu kabisa na kutoa machozi.

"Yo Tim, bado siamini nilitengeneza ngoma kwenye album yangu 'Wild Thoughts' na RiRi. bado siamini. Unajua huwa nalia machozi kila nikiisikia ngoma hiyo? alisema Khaled.

Kwenye kiwanda cha Bongo fleva, msanii yupi ni kiboko yako kiasi anaweza kukutoa akili siku mkikutana na akakusifia?

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments