Dk. Malecela amjibu Makonda asema kushangilia mapema kabla ya Corona kuisha kunaweza kusababisha shidaMkurugenzi wa kitengo cha kuzuia Magonjwa yasiyo ambukiza wa Shirika la Afya Dunia (WHO), Dk. Mwele Malecela, amemjibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusiana na kauli yake aliyoitoa.

Jana Makonda amesema wenye hoteli, mabaa, makampuni na biashara watarudi kazini ifikapo jumapili huku akiwataka watu wapige shangwe kwa kuwa Mungu amewashindia kwenye ugonjwa wa Corona.

Baada ya taarifa hiyo Dk. Malecela amemuambia Makonda hayo yangefanyika angalau baada ya siku 30 ya kutokuwa na ugonjwa hata mmoja.

“Je siku 30 zimepita bila mgonjwa? Kushangilia mapema kunaweza kule shida. Mungu ni mwema lakini pia tutumie vizuri hekima aliyotupatia,” aliandika Dk. Malecela.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments