5/30/2020

Dkt Kikwete Ashangazwa na Msukuma Aliyefukuzwa Ikulu Kisa Mayai ya TausiRais wa Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, ameonesha kushangazwa na maamuzi ya Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli, baada ya kumfukuza mfanyakazi Msukuma wa Ikulu, ambaye alishindwa kununua incubator ya kutotoa mayai ya Tausi.


Dkt Kikwete ameyabainisha hayo leo Mei 30, 2020, jijini Dodoma, wakati wa zoezi la kukabidhiwa ndege aina ya Tausi kwa Marais wastaafu pamoja na mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere.

"Mimi ndiyo mdogo nasema kwa niaba ya Wazee hawa, tunatoa shukrani kwa moyo wako wa upendo kwa kutupatia hawa ndege, tulikuwa tunawatamani lakini ukitoka nao, ukafika nao Msoga, watu watasema amepora, pia nakupongeza kwa maamuzi ya incubator lakini yule Msukuma sikukuambia umfukuze, lakini nilieleza tu masikitiko yangu" amesema Dkt Kikwete.

Aidha awali wakati akizungumza, Rais Magufuli amewapongeza Marais wote Wastaafu walioshiriki kuwatunza Tausi hao.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

1 comment:

 1. Jakaya, wala usishangae.
  Huyu ndiye JPM. Msg sent and Deivered.

  Hana cha Msukuuma mwenzagu wala mtoto
  wa mjomba.

  Huku perform, U R OUT.

  Tumuombee Allah amlinde kipenzi chetu
  halafu furaha ilioje yuko kwetu DOM..

  ReplyDelete

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger