5/28/2020

Donald Trump Afunguka Kuhusu Mauaji ya George Floyd..."Hakika Haki Itapatikana...."


Rais Donald Trump ameahidi haki itapatikana kwa George Floyd, Mmarekani mweusi ambaye aliuawa hadharani mapema wiki hii mara baada ya askari kumkandamiza na goti shingoni.

Trump ametaka haki ipatikane, jana kupitia twitter ameandika

"Kwa ombi langu, FBI na idara ya Haki tayari wapo kwenye uchunguzi wa mauaji haya ya kusikitisha ya George Floyd yaliyotokea Minnesota. Nimewaomba uchunguzi huu uwe makini na nitoe pongezi kwa kazi nzima iliyofanywa na vyombo vya dola vya ngazi ya chini. Moyo wangu nauelekeza kwa familia ya George na marafiki. Haki itapatikana." aliandika Trump kwenye Twitter.

Tamko hilo la Trump limekuja kufuatia maandamano ambayo yamefanyika jana kwenye mitaa ya Minneapolis ambapo wananchi walisikika wakihitaji haki itendeke na hatua kali zichukuliwe kwa maofisa wa polisi waliotenda mauaji hayo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger