5/28/2020

Harmo Afunguka Kutoa Ahadi Hewa HospitaliKONDE Boy, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ au Harmo amefungukia madai ya kutoa ahadi hewa ya kusaidia hospitali mbalimbali na shule kisha kuingia mitini.

 

Harmo alikwaa skendo hiyo hivi karibuni alipokuwa amekwenda nyumbani kwao Mtwara, ambapo alipata nafasi ya kutembelea shule na hospitali mbalimbali mkoani humo na kuahidi kwamba atatoa misaada ya vitu mbalimbali.

 

Baada ya kimya kirefu kupita, baadhi ya mitandao iliibua suala hilo na kudai kuwa Harmo amefanya ‘uswahili’ kwa kuahidi kusaidia hospitali mbalimbali na shule mkoani humo kisha kutotekeleza.“Harmo hajui kama ahadi ni deni.

 

Mwenzake Diamond (Nasibu Abdul Juma) aliwahi kufanya hivihivi Sumbawanga, matokeo yake akachafuka tu,” alichangia mdau mmoja mtandaoni.

 

Akizungumza kwa niaba ya msanii wake, meneja wa Harmo, Beauty Mmary ‘Mjerumani’ alisema ishu hiyo aliiona kwenye mitandao, lakini si kweli kwamba msanii wake alitoa ahadi bandia.Alisema, kilichotokea baada ya kuahidi wakati wanataka kwenda kutekeleza, walipata dharura ya kikazi, hivyo wakalazimika kumuachia mkuu wa wilaya ndio agawe misaada hiyo ambapo zoezi hilo lilishafanyika na msaada wake umeshafika eneo husika.

 

“Tulipata dharura, sasa watu kwa kuwa hawakuona picha sisi tukikabidhi, wakadhani labda pengine tuliingia mitini, kitu ambacho si cha kweli.

 

Wahusika tuliowakusudia tuliwapa misaada yao na ndio maana unaona wanaozungumza ni watu wa mitandaoni ambao hawajui kitu, wahusika hawajalalamika popote,” alisema Mjerumani.

 

Stori na Memorise Richard, Risasi


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger