5/25/2020

Ifahamu Tamaduni Hii ya Kupasua Midomo


Jamii moja katika kisiwa cha Phuket  kusini mwa Thailand imeendesha tamasha la kitamaduni na la kidini linalojulikana kwa jina la ‘Taoist’ kwaajili ya kujitakatisha dhidi ya madhambi, ambapo washiriki husheherekea kwa kujichoma mishale, visu  na mapanga katika mashavu yao.


Tamasha hilo lenye asili ya China hufanyika mwezi Oktoba kila mwaka, ambapo tamasha la mwaka huu limefanyika kuanzia 9, Oktoba likihudhuriwa na jamii kubwa ya Wachina wanaoishi katika eneo hilo .

Moja ya matukio ambayo hufanyika katika tamasha hilo ni pale ambapo mtu mmoja hujichoma visu vingi vikali katika mashavu yake na mwingine hushikilia kichwa chake na kukata ulimi wa mtu huyo kwa kutumia shoka, na kumwacha akibubujikwa na damu kifuani.

“ Watu hao waliokatwa vitu vikali ni miungu ambao hutembea ardhini wakionesha miujiza yao pamoja na vipande vya nyama vilivyokatwa, ili madhambi ya watu wao yasafishwe”, amesema Pathompong Reanthong, ambaye ni mmoja ya waandaaji.

“ Malengo ya sherehe hii ni kwaajili ya watu kuona imani zao, na kujiepusha na matumizi ya nyama. Ni sherehe ya kuondoa mambo mabaya ”, ameongeza.

Washiriki wa sherehe hiyo hawaruhusiwi kula nyama wakati wa mashindano. Kwa mujibu wa washiriki, sherehe hiyo huwakumbusha mwaka 1825 ambapo wageni wa kwanza raia wa China katika eneo hilo walipitia matukio hayo.

Jamii hiyo inaamini katika milo ya mboga za majani na matunda, ikiwa ni katika namna ya kuboresha afya zao.

Kupita juu ya makaa ya moto ni njia ya mwisho kabisa kwa washiriki wa tamasha hilo, tukio ambalo ndilo linalotarajia kuhusisha maelfu ya watu.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger