5/28/2020

Instagram watanagaza rasmi kuanza kulipa video za IGTV


Kwa mara ya kwanza katika historia yake, Mtandao wa Instagram upo mbioni kuanza kuweka matangazo kwenye video za IGTV , na kuwapa fursa watumiaji wake kuanza kutengeneza pesa .Kwa mujibu wa Hollywood Report , kampuni hiyo inataka kutambulisha Updates na Features mpya ambazo zinawanufaisha na kuwafanya watumiaji wake wajitengenezee pesa Kama ilivyo kwa YouTube .

Imeelezwa kuwa Instagram itashiriki kwa kukata asilimia 55 kutoka kwa muhusika wa Content husika Justin Osofsky, COO wa Instagram, amesema kuwa Lengo la kufanya hivyo ni kujaribu kupanua kkampuni na kuifanya kuwa na watumiaji wengi zaidi duniani.Moja Kati ya mabadiliko hayo makubwa , ni pamoja na kuweka matangazo kwenye video ndefu zinazozidi sekunde 60 (InstagramTv) . Pamoja na Beji za makampuni kwenye Insta Live , ambazo zitamfanya aliyeweka video hizo kulipwa.Mbali ya malipo hayo COO bwana Justin Osofsky ametoa ufafanuzi juu ya maudhui ambayo yatakuwa yanawekewa matangazo kwa ajili ya malipo ya muhusika na kutolea mfano maudhui ambayo mtandao wa Ypoutube haulipii ingawa amesema kuwa Insthram itajitahidi kuwa na malipo makubwa kuliko Youtube, “Kama ilivyokuwa kwenye mtandao wa Youtube maudhui ambayo huwa yanafanyiwa malipo ni yale ambayo ni ya muhusika sahihi na baadhi yao ni yale ambayo yatakuwa hayana lengo zuri kwa jamii mfano kutumia vibaya picha za watoto na zile video za ngono.”


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger