5/22/2020

Kenya kufikia kilele cha maambukizi baina ya Agosti na SeptembaJanga la corona bado linajidhihirisha kuwa changamoto katika mataifa mengi duniani. Kenya nayo haijaachwa. Katika siku za hivi karibuni, imekuwa ikirekodi waathiriwa wengi zaidi waliopata maambukizi ikilinganishwa na awali. 

Hata hivyo, Wizara ya Afya nchini humo imetahadharisha kwamba wananchi wajiandae kwa idadi ya juu zaidi ya maambukizi ya kila siku na kusisitizia kuwa kilele cha ugonjwa wa Covid-19 kulingana na mwenendo wake kwa sasa hivi kitarajiwe Agosti na Septemba. 

''Tunatabiri kwamba kilele cha ugonjwa huu kwetu, kitakuwa miezi ya Agosti hadi Septemba ambapo tutakuwa tunarekodi waathirika karibia 200 kwa siku, hilo ni ikiwa tutaendelea na hatua tulizoanza kuzitekeleza hii leo'' 

Kenya inapanga kuanza kupima watu zaidi ya 3,000 kwa siku kuanzia hivi karibuni. Hilo linajitokeza wakati ambapo wizara ya afya imedokeza kuwa na vifaa vya kutosha vya kupima virusi vya corona ambavyo vinaweza kudumu hata kwa mwezi mzima.

Mkurugenzi wa Afya ya Umma Patrick Amoth, alisema maambukizi yameingia katika ngazi ya kijamii. 

''Kwa kiwango cha upimaji tunacho lenga, tunaona idadi ikiongezeka lakini hili halifai kuwatia wasiwasi...'' 

Katika tangazo la kila siku kuhusu virusi vya Covid-19, Waziri wa Afya nchini humo Bwana Mutahi Kagwe, Alhamisi 21, 2020 alisema jumla ya watu waliopata virusi vya corona imefikia 1,109, huku 80 wakibainika baada ya kupimwa kwa sampuli 3,102. 

Aidha bwana Kagwe aliweka wazi kwamba idadi inayoongezeka kila siku ni ishara tosha virusi hivyo vinazidi kusambaa kila uchao. 

''Kadiri tutakavyopima watu zaidi, ndivyo tutakavyofahamu virusi hivi vimesambaa kwa kiwango gani.'' 

Aidha wizara hiyo imesema inaazisha maabara nyengine mbili ili kupima vipimo vya watu wanaopimwa katika mpaka na Tanzania na eneo la mlima Kenya. 

Lakini je hili litaathiri vipi mfumo wa masomo? 

Kumekuwa na mjadala kuhusu ni lini taasisi za elimu zifunguliwa tena. 

Wizara ya elimu imeunda jopo kuthathmini hali na kutoa mapendekezo yake. 

Chama wa waalimu KUPPET nchini humo kimependekeza Juni 15 taasisi kuanza kufunguliwa taratibu kulingana na wale wataokafanya mitihani yao ya kitaifa mwaka huu lakini vilevile, kwa kuzingatia mwongozo wa wizara ya afya . 

Hata hivyo pendekezo hilo limepata upinzani hasa kutoka kwa chama cha wazazi chenye kutofautiana na msimamo huo, kikidai kwamba kilipokea maoni ya wazazi ambao bado wanahofu kuhusu suala hilo wakidai kwamba ni mapema mno na watakuwa tayari watoto kurejea mashuleni iwapo tu virusi hivyo vitakabiliwa. 

Dr Agumba Ndalo mtaalamu wa elimu nchini Kenya anasema 

''Tusiharakishe kufungua vyuo vya elimu kama bado kesi za corona zinazidi kama hapa kenya'' 

Daktari huyo anasema mara nyingi shuleni huwa kuna idadi kubwa ya watoto na pia kawaida kuna tatizo la kubadili tabia kwa haraka na pengine kufunguliwa mapema kwa taasisi hizo kunaweza kusambaza virusi vya corona hata zaidi. 

Pia amegusia wasiwasi wa kujenga kinga ya mwili yenye uwezo wa kukabiliana na maambukizi hayo na hofu ya uwezo wa hospitali kudhibiti maambukizi iwapo yatakuwa ni yenye kupita kiasi. 

Licha ya kwamba baadhi ya shule sasa hivi zinatumika kama vituo maalum vya karantini, shule nyengine huw idadi kubwa ya watu, madarasa machache na hata usafi unaodumishwa siyo wa kuridhisha. 

Hata hivyo Wizara ya Afya Duniani- WHO, ilisema kuwa kuna haja ya kujua namna ya kuishi na janga hili kwasababu kuna uwezekano mkubwa ugonjwa wa Covid-19 ukuchukua muda mrefu zaidi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger