5/22/2020

Leo ukipiga chafya imekuwa hukumu, zamani ilikuwa ni afya" - Polepole


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole, amesema kuwa chama chake kimekaa na kutafakari kwa muda, kufuatia hofu iliyojengeka kwa wananchi iliyopelekea hata ikifikia hatua ya kupiga chafya, lazima mtu ajifikirie na kumpongeza Rais Magufuli kwa maono yake makubwaPolepole ameyabainisha hayo leo Mei 22, 2020, Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za chama hicho zilizopo Lumumba, na kusema kuwa isingekuwa maono ya Rais Magufuli ya kuzuia kila mtu kutoa taarifa za ugonjwa wa Corona, basi hali isingekuwa nzuri.

"Chama kilikaa muda kikatafakari kikasema, hivi si tumekua maisha yetu yote mtu akipiga chafya tunamuambia afya!, leo ukipiga chafya imekuwa ni hukumu unaweza ukachukuliwa hatua, tukaseme tujiongeze tuchukue hatua, na ndiyo maana hata hili jambo la kufungia watu ndani kama mifugo, Mataifa makubwa wananchi wanaandamana" amesema Polepole. 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger