Majambazi saba yauwawa Dar, Mambosasa awataka ndugu kwenda kutambua maiti Muhimbili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, amewataka wale watu ambao wana ndugu zao majambazi na wanajua kabisa walienda kutafuta lakini hawajarudi, basi waende Muhimbili kwa ajili ya kutambua miili ya ndugu zao. 

Hayo ameyabainisha leo Mei 25, 2020, wakati akitoa taarifa za majambazi saba waliouawa wakati wa majibizano ya risasi na Polisi usiku wa kuamkia leo, waliokuwa wakielekea kufanya ujambazi katika ghala la GS Group Limited, ambapo kwa bahati mbaya majambazi hao majina yao hayakuweza kufahamika. 

"Kama unavyoelewa hakukuwa na mahojiano kati ya Jeshi la Polisi na wahusika, walipoona wanafuatiliwa walianza kukimbia, walianza kusalimia kwa kurusha risasi na Askari wakajibu, mpaka sasa sina majina ya wahusika lakini mtu yeyote anaweza kwenda Muhimbili kwa ajili ya kutafuta kama anajua, kuna ndugu yake jambazi haonekani alienda kuvuna ameshindwa kurudi, basi aende Muhimbili ataweza kumtambua ndugu yake" amesema Kamanda Mambosasa. 


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera Kamanda kanda Maalumu.
    Tunaitaka Dar'Salam yetu kama Jina lake

    Endeelea Kudumisha Usalama na Amani.

    Viashiria na vitendo vya kuvunja Amani
    na Utulivu hatuna simile navyo.

    Kabla ya Uchaguzi na hata Baada.

    Hongereni sana vyombo vya ulinzi na Usalama na Raia wema.

    Eid Mubarak..!!

    ReplyDelete

Top Post Ad