Mamba Alienusurika Mabomu ya Vita ya Pili ya Dunia Afariki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mamba alienusurika Vita Kuu ya Pili mjini Berlin na ambaye kulikua na tetesi- zisizo za kweli- kwamba alikua ni wa kiongozi Nazi leader Adolf Hitler amekufa katika hifadhi ya wanyama iliyoko mjini Moscow.

"Jana asubuhi, mamba huyo aliyefahamika kama Mississippi Saturn alikufa kutokana na uzee. Alikuwa na umri wa miaka takriban 84 - umri wa kuheshimiwa sana ," ilisema hifadhi ya wanyama.

Saturn alitolewa kama zawadi kwa hifadhi ya wanyama ya Berlin mwaka 1936 muda mfupi baada ya kuzaliwa nchini Marekani. Alitoroka hifadhi ya wanyama baada ya kupigwa mabomu mwaka 1943.

Wanajeshi wa Uingereza walimpata miaka mitatu baadae na kumtoa kwa Muungano wa Usovieti.

Jinsi alivyoishi miaka yote hiyo limesalia kuwa ni jambo la muujiza, lakini tangu Julai, 1946 mamba huyo amekuwa akitembelewa sana na wageni mjini Moscow.

"Hifadhi ya wanyama ya Moscow imekuwa na heshima kubwa ya kumtunza Saturn kwa miaka 74 ," imesema katika taarifa yake.

"Kwetu sisi Saturn alikua ni enzi nzima, na hilo sio la kutia chumvi hata kidogo… Alituona wengi wetu tulipokua watoto. Tunatumai kuwa hatukumkatisha tamaa ." 

Mamba huyo wa Mississippi kwa kawaida huishi kati ya miaka 30 na 50 na msituni, iliongeza kusema taarifa kuhusu kifo chake. 

Saturn huenda akawa ndiye mamba aliyekuwa na umri mkubwa zaidi duniani- haiwezekani kusema hilo. Mamba mwingine dume, aliyefahamika kama Muja ambaye yuko katika hifadhi ya wanyama ya Belgrade nchini Serbia, pia ana umri wa miaka 80 na zaidi na bado anaishi. 

Lakini bila shaka hakuna mamba mwingine anayeweza kushindana na Saturn inapokuja katika suala la kuuza kumbukumbu za matukio yao. 

Taarifa yake iliyogonga vichwa vya habari na kuvutia wengi ilikua ni kuhusu maelezo ya tetesi za uvumi kwamba alikuwa ni mmoja wa wanyama binafsi wa Hitler , jambo ambalo lilikua si sahihi. 

"Muda mfupi baada ya kuwasili kwa mnyama huyo, uvumi ulijitokeza kwamba alikuwa ni mmoja wa wanyama wa Hitler, na sio kutoka katika hifadhi ya wanyama ya Berlin," Shirika la habari la Interfax liliripoti. 

Haijawa wazi ni vipi tetesi hizo zilianza. 

Hifadhi ya wanyama ya Moscow ilipuuzilia mbali ripoti za aina hiyo, ikasema wanyama ''sio wanasiasa na hapaswi kuwajibishwa na madhambi ya binadamu ".

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad