Ticker

6/recent/ticker-posts

Mbunge Selasini Afunguka Chanzo Cha Kifo cha Dkt. Masumbuko

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPAMbunge wa Rombo kupitia CHADEMA Joseph Selasini, amemzungumzia kwa kina Kaka yake ambaye alikuwa Mwanasheria na Mhadhiri Dkt Masumbuko Lamwai na kusema kuwa afya yake ilidhoofika kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita na baadaye akashikwa na Malaria kabla ya umauti kumfika.

Selasini ameyabainisha hayo leo Mei 5, 2020,  na kusema kuwa licha ya kusumbuliwa na Malaria, lakini alikuwa akiendelea kupata dawa hadi hali yake ilipobadilika tena jana usiku na kukimbizwa Hospitali.

"Afya yake ilidhoofu katika kpindi cha wiki mbili zilizopita lakini pia alipigwa na Malaria kali ambayo alikuwa anaendelea kupata dawa, hata Jumapili alikaa na watoto wake wakaongeaongea sana ni kwa vile tu mtu huwezi kujua Mungu amepanga uondoke saa ngapi, jana usiku ndiyo akazidiwa na akafariki njiani wakati anapelekwa Hospitali, mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Lugalo" amesema Selasini.

Mbunge Selasini ameongeza kuwa, Kaka yao huyo alikuwa ndiye kiongozi wa familia na hata baada ya wazazi wao kufariki, yeye alibaki kuwa nguzo kwa kuwaongoza kwa hekma na busara.

Aidha wakati wa uhai wake Dkt Lamwai, licha ya kuwa Mwanasheria pia aliwahi kuwa Diwani wa Manzese na hatimaye kuwa Mbunge wa Ubungo, aliwahi pia kuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaa na Chuo Kikuu cha Tumaini kanda ya Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments