Unaambiwa Mike Tyson Anazeeka na NGUMI zake..Apewa Mabilioni ya PESA Kurudi Ulingoni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Unaambiwa Mike Tyson Anazeeka na NGUMI zake..Apewa Mabilioni ya PESA Kurudi Ulingoni

Jina la Mike Tyson limeanza tena kuandikwa upya kwenye headlines za dunia, ni baada ya kutangazwa uwepo wa pambano la hisani kati yake na Evander Holyfield.

Sasa fahamu kwamba jina la Mike Tyson (53) linaweza kuendelea kuandikwa zaidi kwani imetoka taarifa kwamba mbabe huyo wa zamani wa masumbwi ya uzito wa juu duniani alipewa ofa ya ($20M) sawa na Bilioni 46.2 za Kitanzania kurejea ulingoni kwa pambano moja tu.

Kwa mujibu wa MMA Fighting, bondia huyo ambaye alistaafu mwaka 2005 aliahidiwa ofa hiyo kwa pambano moja la kampuni ya ngumi iitwayo (Bare Knuckle Championship) lakini aliipiga chini.

Rais wa kampuni hiyo bwana David Feldman amesema anaamini Tyson ataikubali tu ofa yao na milango bado ipo wazi ya kukubali.

Hadi anatundika Glovu zake, Mike Tyson alikuwa amepigana mapambano 58, akishinda 50 huku 44 ikiwa kwa KO, na alipoteza mapambano 6 na mawili yakimalizika bila mshindi kwa sababu maalum.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad