Mr. Blue Amefunguka Kuhusu Msaada Mkubwa Aliowahi Kupewa na Mtangazaji Bdozen "Nilikuwa Nataka Kuacha Mziki"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mr. Blue amefunguka kuhusu msaada mkubwa aliowahi kupewa na Mtangazaji Bdozen.

Kwenye mahojiano na XXL leo, amesema kipindi anapitia magumu ya kumpoteza mama yake mzazi na hata baada pia ya kumpoteza mtayarishaji ambaye aligundua kipaji chake Roy Bukuku wa G Records, Blue alikata tamaa na mazito ya dunia hadi kufikia maamuzi ya kutaka kuacha muziki kabisa.

Lakini baada ya kukutana na @bdozen na kumsikilizisha wimbo wa PESA, Dozen aliikubali ngoma hiyo na alimwambia Byser aiachie kwanza halafu ndio aache muziki.

"Nikushukuru sana wewe B12 na nakuombea sana Mungu kila siku azidi kukubariki kwa sababu nilifikia time nikataka niache muziki, nakumbuka na wewe nikakufata nikiwa na wimbo wangu PESA, ukaniambia niutoe tu huo wimbo halafu niache muziki." alisema Mr. Blue.

Kumbukumbu za @mrbluebyser1988 zinatueleza kwamba baada ya kumpatia wimbo huo Dozen, hakuusambaza mahali popote kwani alikuwa kwenye msimamo wake wa kuacha muziki, lakini kilichofata baada ya wimbo kusikika ni historia.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad