5/28/2020

Mwanaume Alazwa Hospitali Kwa Kula Pilipili ‘Kali zaidi’ Duniani

Mwanaume mmoja ambaye ni raia wa Marekani amejikuta akiumwa kichwa sana pamoja na shingo hadi kulazwa hospitali kutokana na kula pilipili kali zaidi duniani ijulikanayo kama “Carolina Reaper” kwenye mashindano.

Inaelezwa kuwa mwanaume huyo alishindana kwenye mashindano ya kumtafuta bingwa wa kula pilipili hiyo kali, jambo lililomsababishia magonjwa hayo.

Madaktari wameeleza kuwa, kula pilipili za aina hiyo kunaweza kusababisha mgonjwa kuugua kichwa kwa hadi kipindi cha wiki tano, hivyo ni vyema watu kuchukua tahadhari hiyo.

Mwanaume huyo baada ya kufanyiwa uchunguzi hospitali ilgundulika kuwa mishipa ya artery kwenye ubongo wake ilikuwa myembamba kwamuda mfupi jambo lililopelekea kichwa chake kuuma kwa namna isiyo ya kawaida.

SOMA PIA: Nafasi Mbili za Ajira Kazini Kwetu LTD
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger