5/30/2020

Nandy Atangaza Watu Anaowataka Kwenye Ndoa yake


Msanii Nandy The African Princess amesema, siku ya ndoa yake na Billnass watahitaji idadi ya wahudhuriaji 300 au 400, kwa sababu hataki kufunga ndoa ya watu kumi kisa kuogopa Corona.

Nandy ameeleza hilo kwenye show ya Dadaz ya East Africa TV, ambapo amefunguka mengi ikiwemo suala la mahusiano, kazi, bifu na wasanii wa kike, pamoja na historia yake ya muziki.

"Alivyonivalisha pete wiki nzima ilikuwa ni furaha na kupewa hongera tu, huku marafiki zangu na wake walikuwa wapo tayari kutoa michango ya harusi, kipindi tumeachana Billnass aliniambia ikitokea tunarudiana tutafunga ndoa moja kwa moja, hata ile kunivisha pete nilikuwa sijatemegea kama ingetokea mwaka huu, nataka harusi yangu iwe na watu 300 au 400 sio ya watu wachache kisa kuogopa Corona" ameeleza Nandy.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger