Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Nuh Aeleza Sababu ya Kuwa na Tattoo ya Mke wa Mtu Aliyoichora

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Msanii wa BongoFleva Nuh Mziwanda, amenyoosha maelezo kuhusu kuendelea kuwa na tattoo yenye jina la "Shishi Baby" ambaye alikuwa mpenzi wake wa zamani na sasa ni mke wa Uchebe.

Akitoa maelezo hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, Nuh Mziwanda amesema ana tattoo nyingi sana mwilini mwake na hajawahi kujutia kuchora kwa sababu ni kitu ambacho anakipenda.

"Mimi nina tattoo nyingi sana na nazipenda sichori kwa kuiga, kuhusu Shilole ni tattoo sio mwanamke, niliichora ukweli sikulazimishwa nilifanya hivyo kutoka ndani ya moyo wangu na nilikuwa najua kama kuna kuachana au kugombana, sikuchora kwa sababu ya kuwaonesha watu na kipindi nachora hakuwa mke wa mtu" amesema Nuh Mziwanda.

Post a Comment

0 Comments