5/30/2020

Rais Mstaafu Mwinyi Ashindwa Kujizuia Ampa Tano Rais Magufuli...Unafanya Mambo Mapya na Makubwa: Mwinyi Amwambia MagufuliRaisi mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi amempongeza sana Raisi John Magufuli kwa kufanya mambo mengi, mapya na mazuri.

Akisalimia wananchi wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi za ikulu Dodoma, mzee Mwinyi amesema Rais Magufuli anatumia fikra za ujana kufanya mambo makubwa nchini.

Baadhi ya mambo mapya na makubwa aliyofanya Raisi Magufuli ni kuhamishia serikali na wizara zote Dodoma na kujenga ikulu mpya Dodoma.

Raisi Magufuli pia anajenga mradi mkubwa wa umeme unaoitwa Mwalimu Nyerere Hydro power Project wenye zaidi ya megawati 2000 katika bonde la Rufiji.

Rais Magufuli pia amewasha umeme katika zaidi ya vijiji elfu nane tangu aingie madarakani.

Kama hiyo haitoshi Rais Magufuli yupo anajenga treni ya mwendo kasi kutoka Dar es salaam mpaka Mwanza ambapo kipande cha kwanza kutoka Dar es salaam hadi Morogoro kitazinduliwa hivi karibuni.

Yapo mengi amefanya Raisi katika kipindi cha miaka mitano angani, ardhini na majini ila nafasi haitoshi kuandika vyote hapa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi 25 kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi kwa ajili ya kuwafuga katika makazi yake. Hafla ya Makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

1 comment:

 1. Alhajj Ali Hassan, Mcha mungu na msema
  kweli Alie na Busara na Hekima.

  Babba Ruksa, Swadakta kwa Magu wetu
  yote uliyo sema.Ana Maono na Uthubutu.

  Mwenyezi mungu akupe Afya na Atulindie
  kipenzi chetu Performance Driven Magu.

  ReplyDelete

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger