5/22/2020

RC Makonda atoa siku 10 kwa uongozi wa Manispaa ya Kigamboni


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa siku kumi kwa uongozi wa Manispaa ya Kigamboni kuhakikisha Hospital hiyo inaanza kutoa huduma kwa wananchi ifikapo June Mosi baada ya Majengo yote ya Hospital hiyo kukamilika.RC Makonda ametoa agizo hilo leo wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Wilayani humo ambapo pia amekabidhi Magodoro 175, Mashuka 1,294 na Ndoo na kueleza kuwa ifikapo Jumanne ya wiki ijayo atakabidhi tena Mashine mbili za Ultrasound zenye thamani ya Milioni 70 na Vitanda 100 ili kuhakikisha huduma zinaanza kutolewa.

Aidha RC Makonda amemuelekeza Mganga Mkuu wa Mkoa huo kuhakikisha anapeleka Watumishi 40 kwenye hospital hiyo kwaajili ya kutoa huduma ili kutimiza lengo la Serikali ya Awamu ya Tano la kupunguza kero za Afya kwa Wananchi.

Akiwa katika Ukaguzi wa Ujenzi wa Barabara na Round about inayounganisha barabara za Kuelekea Feri na Kibada Kutokea Daraja la Mwalimu Nyerere
RC Makonda amewaelekeza TARURA na TANROAD kuhakikisha ujenzi wa Barabara na Mzunguko wa Magari vinakamilika na kukabidhiwa kabla ya Mwezi September Mwaka huu.

Pamoja na hayo RC Makonda amewaelekeza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Watendaji wa Jiji hilo kuhakikisha maelekezo na Ahadi zote zinazotolewa na Rais Magufuli vinatekelezwa kwa Wakati pasipo kushurutishwa huku akiwataka wakandarasi wote kuhakikisha miradi yao inakamilika kwa wakati.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger