5/21/2020

Tulionya Tukapuuzwa, Laana ya Dr. Slaa ni KaliMwaka 2015 wakati Dr Slaa anaondoka chadema, sisi wenye uwezo wa kuona mbali tulionya kwamba chadema imetema big g na kuchukua karanga za kuonjeshwa(Lowasa), Kama kawaida ya bavicha badala ya kujibiwa kwa hoja tukaishia kutukanwa.

Ikumbukwe ndani ya ujenzi wa chadema kuna damu ya Dr Slaa alivunjwa mkono na mke wake alipigwa hadi mimba kutoka akiipigania chadema!

Lakini baada ya Mbowe kubadili gia angani na kuuza chama kwa Lowasa, Bavicha waliibuka na matusi na kejeli nyingi kwa Dr Slaa kwamba mwacheni aende tu hana faida yoyote chadema.
Kuna bavicha wengine walifikia hatua ya kumbatiza jina la dr Mihogo ili tu kuhakikisha wanamwondolea heshima yote mzee huyu kipenzi cha wapenda haki na wazalendo wa nchi yetu.

Dr Slaa aliikuta chadema ina wabunge 4, tu lkn kwa juhudi zake, kujitoa kwake chadema ikapaa hadi kuwa na wabunge wa majimbo 30+ lakini hilo halikuwafanya bavicha waone soni kumvurumishia matusi mzee huyu.

Leo baada ya miaka 3 tu ya kuondoka Dr Slaa , Chadema iko hoi taabani.!
Chadema ya leo haina mvuto kwa wananchi na imepauka Kama shati,
Chadema ya leo inakimbiwa na madiwani na wabunge wake kisa udikiteta wa mbowe wa kuibadilisha chadema kutoka taasisi hadi kampuni binafsi.

Bavicha waliofunzwa kumtukana Dr Slaa na kumtukuza Edward Lowasa, sasa wanajuta.

Laana ya kumtukana Dr Slaa ndani ya miaka 3 imewatafuna kweli kweli na sasa wanajuta.
It is too late.!

By Etwege
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger