5/25/2020

Upinzani Bongo Wazidi Kupurutika...Katibu wa CHADEMA Tarime atimkia CCM

Na Timothy Itemba, Mara

SIKU Chache  baada ya mwenyekiti wa Chama cha Demokorasia na maendeleo Chadema aliyekuwepo,Mwita Jodeph kuhama chama chake na kujiunga na Chama cha mapinduzi CCM katibu wake leo amejiengua  na kufuata Nyayo zake ambapo amekihama Chama cha Chadema na amejiunga na Chama cha mapinduzi.


Wengine walihama na kujiunga na Chama cha mapinduzi leo ni pamoja na Bonifasi Mataro Mwita ambaye alikuwa mwenyekiti kata ya Matongo kupitia Chadema,Geoger Nyanchama aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji cha Kyasangura kupitia Chadema,Emanuel Marwa Magige aliyerkuwa mwenyekiti kata ya Nyandoto kupitia Chama cha ACT Wazalendo,Nashoni Mchuma ambaye alikuwa mgombea udiwani kata ya Gwitiryo kupitia Chadema mwaka 2015.


Akiwapokea mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya Tarime,Daudi Marwa Ngicho alisema kuwa wapinzani kwasasa hawana nafasi Tarime na uchaguzi ujao watafute kazi ya kufanya viongozi waliopo kwenye nafasi kama vile John Heche Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini na Esther Matiko Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini bdala ya kugombea nafasi walizo nazo waende wakauze mayai.

Ngicho aliongeza kuwa CCM Tarime imeimarika tofauti na miaka mingine yote hiyo nikwasababu ya utendaji kazi wa Rais wa awamu ya Tano John Pombe Magufuli akiwemo mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM Wilaya Tarime,Daudi Marwa Ngicho bila kumsahahu Naibu Waziri TAMISEMI,Mwita Waitara ambapo wananchi wanaona  kazi wanazozifanya na wakiwaunga mkono.

Katibu wa CCM Wilaya Tarime,Kamisi Mukaruka Kura alisema kuwa Chadema Tarime imepata pigo kukimbiwa na viongozi wa ngazi ya juu akiwemo katibu na mwenyekiti,na kuwa hizo ni juhudi za Raisi John Pombe Mgufuli za utendaji kazi wake wa kuwaletea wananchi maendeleo na kusimamia Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015-2020.

Naye Naibu waziri Tamisemi Mwita Waitara alisema kuwa hali ya Chadema itaendelea kuwa mbaya wilayani Tarime na Tanzania kwa ujumla kutokana na watu kuendelea kujitambua na kutambua shuguli anazozifanya Rais John Pombe Magufuli ambazo kwa ujuma zinatangaza hali ya hatari kwa vyama pinzani huku wanachama wake wakichukua nafasi ya kuvihama vyama vyao na kujiunga na Chama cha mapoinduzi CCM.

“Kama unataka kufanya Siasa njoo Chama cha mapinduzi ili ukafanye Siasa na kama unataka kuzurura ndani ya vyama nenda vyama vingine kazurure,Rais wetu anafanya kazi kubwa ya maendeleo kwa Wananchi hususani kwenye janga hilli la Corona Rais wetu amepata umaarufu mkubwa ndani ya Nchi na mataifa mengine hususani pale ambapo aliwajali watu wake wa hali ya chini kutowafungia ndani huku  kufa kwa njaa badala yake aliwataka Watanzania kwendelea kuchapa kazi huku akimtanguliza mwenyezi Mungu katika hilo”alisema Waitara.

Aliyekuwa katibu wa Chama cha Demokorasia na maendeleo Chadema wilaya Tarime,Samweli Mgaya Nyandula aliyehamia CCM alisema kuwa amehamia Chama cha mapinduzi kwa matakwa yake mwenyewe bila kulazimishwa na mtu Walakushawishiwa na Mtu alitumia nafasi hiyo kupongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi kuwa hayo ndiyo walikuwa wakiyapigania wapinzani na sasa yanatekelezwa hana haja ya kubaki Chadema.

Nyandula alikemea tabia ya wapinzani8 kuwatupia lawama wanachama wake ambao wanahama kuwa wamenunuliwa jambo ambalo amesema kuwa yeye binafsi haja nunuliwa na kuwa kama alivyoingia Chadema bila kununuliwa ndivyo ambapo ameingia CCM bila kununuliwa na bila kushawishiwa na mtu yeyote.


Mmoja wa wanachama wa Chama cha Mapinduzi kutoka Jimbo la Hai,Apaisaria Jonadhan  ambaye pia ni mtia nia katika jimbo hilo alisema kuwa wamechoka na Siasa za malumbano kutoka vyama pinzani kwa hali hiyo wananchi wampe kura Rais John Pombe Magufuli katika uchaguzi ujao 2020.

Mwanamama huyo aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kuvuta Fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani wanawake kumekucha ma mijeshi kubwa sasa ni nafasi yao kujitokeza kugombea wasibaki nyuma huku kwakufungwa na mila na misemo hasi ya makabila isiyotaka wanawake kugombea.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

4 comments:

 1. CHADEMA MLIE TUUU.
  HECHE IWE JUA IWE MVUA. NJOO SENGEREMA TUKUPE AJIRA YA KUFUNDISHA SHULE BAADA YA KUHAKIKI CHETI CHAKO.
  NA KAMA NI FEKI UJUE HATUTOKUAJIRI NA TUTAKUFIKISHA ULIPO KUZOEA.
  Magumashi hatuyataki..!!!
  TARIME OYEEEEE..

  ReplyDelete
 2. CHADEMA imekula kwao Tena kwa kiasi kikubwa misicho. A mfano.

  Tumo a kwa marudio Usanii WA Kutoka BUNGENI. A Upingaji WA Miswada ya BAJETI Za. Mikakati ya MAENDELEO.

  Tumeshuhudia nitihada wNazofanya kuhakikisha Chama kilichopo madarakani kwamba mionekane hamimudu Uongozi WA Taifa (Hilo walishindwa KATIKA AWAMU HII ya TANO na wamenaribu kujizolea umaarufu hoja zao zote zika mchwara)

  Sitegemei kama Kuna Mtanzania mwenye ajili timamu ataitoa hata Robo kura yake kwa Genge hi LA Wapiga MAENDELEO.

  WaTanzania WAnacho taka NI MAENDELEO /HUDUMA na Si vinginevyo

  ReplyDelete
 3. Good Morning CDM

  ReplyDelete
 4. Rudisheni comment blog yetu.

  ReplyDelete

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger