Vurugu Marekani Baada ya Mtu Mweusi Kufariki Mikononi mwa Polisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Vurugu Marekani Baada ya Mtu Mweusi Kufariki Mikononi mwa Polisi

Kumekuwa na vurugu na mapambano kati ya polisi na waandamanaji katika mji wa Minneapolis nchini Marekani baada ya kifo cha mwanaume mmoja mweusi akiwa mikononi mwa polisi

Polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi na waandamanaji walirusha mawe na kupulizia mapambo ya graffiti kwenye magari ya polisi.

Kilichotokea kwenye maandamano

Walianza siku ya Jumanne jioni, wakati mamia ya watu walipofika katika eneo ambalo tukio lilitokea, Jumatatu jioni.

Waratibu walijaribu kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani na kuzingatia masharti ya kukaa mbalimbali, waandamanaji waliimga ''siwezi kupumua,'' na ''ingeweza kuwa mimi''.

Mmoja wa waandamanaji Anitha Murray aliliambia gazeti la Washinton Post: ''inaogopesha kuwa hapa wakati wa janga la corona, lakini kwa nini nijiweke mbali?''

Kundi la mamia ya watu baadae waliandamana mpaka kwenye idara ya polisi 3rd Precinct, ambapo maafisa waliohusika na kifo hicho walikuwa wakifanya kazi.

Mtu mmoja alikiambia chombo cha habari cha CBS: ''Hii ni mbaya sana. Polisi lazima watambue kuwa hali hii wameitengeneza wenyewe.''

Polisi wamesema kuwa mtu mmoja amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi lakini taarifa za kina hazijatolewa kuhusu tukio hilo.

Maafisa wanne wa polisi katika jimbo la Minnesota nchini Marekani wamefutwa kazi kufuatia kifo cha mtu mweusi ambaye alikuwa amekamatwa na kuonekana akizuiliwa chini kwa kushikwa shingo.

Afisa mkuu wa polisi katika jimbo hilo Medaria Arradondo amesema kwamba maafisa hao wanne sasa ''sio wafanyakzi wa kikosi hicho''.

Kanda ya video inaonesha, mtu huyo kwa jina George Floyd , akilia na kuwaambia maafisa hao weupe ''siwezi kupumua''.

Kisa hicho kinafanana na kile cha Eric Garner, mtu mweusi aliyefariki akikamatwa na polisi mjini New York mwaka 2014.

Shirika la ujasusi nchini Marekani FBi lilisema litachunguza kisa hicho cha Minneapolis kilichofanyika Jumatatu jioni.

Maafisa wa polisi wa Minnesota walisema kwamba Floyd mwenye umri wa miaka 46 , ambaye alikuwa anafanya kazi kama afisa wa usalama katika mkahawa mmoja alifariki akifanyiwa matibabu kufuatia malumbano na maafisa wa polisi.

Siku ya Jumanne, Meya Jacob Frey alithibitisha kwamba maafisa hao wanne waliohusishwa na kisa hicho wamefutwa kazi. ''Huu ndio uamuzi tuliochukua''.

Katika mkutano na vyombo vya habari mapema, bwana Frey alikitaja kisa hicho kama cha kushangaza.

''Ninaamini kwamba kile nilichokiona ni kitendo cha makosa kwa kiwango chochote kile'' , alisema.

''Kuwa mtu mweusi nchini Marekani hakustahili kuwa hukumu ya kifo''.

Ni madai ya hivi karubuni ya unyanyasaji unaotekelezwa na maafisa wa polisi dhidi ya Wamarekani weusi.

Visa maarufu vya hivi karibuni vinashirikisha afisa mmoja wa eneo la Maryland ambaye alimpiga risasi mtu mmoja akiwa ndani ya gari la kupiga doria.

Kisa hicho cha Minneapolis kilianza baada ya ripoti kwamba mteja mmoja alikuwa anajaribu kutumia noti bandia ya dola 20 katika duka moja.

Afisa huyo alimuona mshukiwa akiwa ndani ya gari lake, mtu huyo alikataa kukamatwa kulingana na maafisa wa polisi.

Waliambiwa kwamba mtu huyo ambaye hajatambulika alikuwa ameketi juu ya gari la rangi ya buluu na alionekana kana kwamba ametumia kishawishi fulani.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hata lini Africa!? Hata lini Africa!?
    Tutaendelea kufumbia macho hayo hadi lini?
    Je hayatuhusu kabisa?!
    Nani basi responsible kupaza sauti na kuchukua hatua (zile zilizo ktk ok uwezo wetu)
    Mbona Mugabe aliwekewa vikwazo?
    Mbona Africa au nchi ya kiafrika ikifanya lolote nje ya interest za magharibi au yahusuyo sexualities actions za maramoja hufanywa na kukemewa?
    Bwana mh kabudi,mwiteni tena huyo mama,mwbieni hatufurahi juu ya mauaji ya waafrica wamarekani.
    Mbona tz ina ok ardhi kubwa tu?
    Kuna ubaya gani kutoa ukaribisho kwa weusi wa America ambao watapendelea kufanya tanzaTannyumbani kwao?
    Wapeni Karibu km watakataa,basi sisi tumefanya yatupasayo kwa Mungu
    Katika kitanbu kitakatifu haturuhusiwi kufumbia macho mateso ya MTU wa damu yetu

    ReplyDelete

Top Post Ad