5/28/2020

Wajawazito acheni kunywa dawa za kienyeji pindi uchungu unapowashika ,mganga mfawidhi kituo cha afya SirariNa Timothy Itembe Mara.

WAJAWAZITO wametakiwa kuacha tabia ya kunywa dawa za kienyeji pindi wanapokaribia kujifungua badala yake waende katika kituo cha Afya kilicho karibu nao.

Mganga mfawidhi katika kituo cha Afya Sirari,Rasulu Daudi alitoa kauli hiyo pindi alipokuwa akipokea msada wa mashuka kutoka kwa madau wa maendeleo Amina Makilagi ambaye ni Mbunge Viti maalumu Tanzania aliyoitoa wakati wa ziara yake wilayani Tarime mkoani Mara.Mashuka hayo taklibani pear 50 yalikabidhiwa na kamati ya Siasa ya chama cha mapinduzi wilaya Tarime wakiongozwa na katibu wa Chama hicho Khamisi Mukaruka maeneo mengine waliyokabidhi msaada huo ni pamoja na Kituo cha Afya Nkende mashuka pear 50 Shule ya sekondari Bomani Kompyuta Tatu na shule ya msingi Gamasara mabati 100.

Mganga huyo akipokea Masada huyo alisema kuwa baadhi ya wajawaito wanakunywa dawa za kienyeji pindi wanaposhikwa na uchungu jambo ambalo nimakosa na wanaposhindwa wanakimbilia kituo cha Afya hali Mtoto amechoka.

 “Mimi niwashauri wajawazito wazingatie mashauri na elimu wanayopewa pindi wanapokuwa wanahudhuria Kiliniki waachae na kunyw adawa za kienyeji pindi wanaposhikwa na uchungu hali hiyo inachangia kuwepo vifo vya mama na mtoto,serikali imepanga kila mjamzito ahudhurie Kilini na mwenzi wake ili linapotokea jambo wakumbushane cha kufanya ”alisema Daudi.

Kwa upande wake katibu wa CCM Wilaya Tarime Khamisi Mukaruka alitumia nafasi hiyo kuwataka viongozi waliomadarakaniu kwenda kutimiza ahadi walizoahidi wakati wanagombea ili kufanya hivyo jamii itamwamini na kumpa kura tene vinginevyo atakuwa amejiharibia kura mwewnyewe.

Mukaruka alisema kuwa msaada huo umetolewa na Mbunge viti maalumu Tanzania ikiwa ni ahadi aliyoahidi wakati wa ziara yake wilayani Tarime.

Naye Diwani kata ya Nkende Danieli Komote alishukuru Rais awamu ya Tano John Pombe Magufuli kuwaletea fedha shilingi milioni 400 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Magena pia diwani huyo alitumia nafasi hiyo kumshukuru mdau Amina Makilagi kuwakumbuka na kutoa msaada wa mashuka katika kituo cha Afya Magena.

Nipende kuwashukuru kamati ya Siasa kufika na kukabidhi mashuka ndani ya kituo chetu cha Afya Magena mashuka haya yataenda kufanya kazi iliyokusudiwa na kwa hali hiyo nipende kuwashukuru wananchi wangu kutoa eneo la kujenga kituo cha Afya pamoja na kuchangia mali zao na nguvu kazi lengo likiwa nikufanikisha alisema Komote.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger