Wanyama 380 Wamekufa kwa Kugongwa na Gari

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wanyama 380 Wamekufa kwa Kugongwa na Gari

WANYAMA 380 wamekufa kwa kugongwa na magari
ndani ya mwaka mmoja 2019 katika eneo la mapito ya wanyama kuanzia
Magugu wilayani Babati hadi Makuyuni
wilayani Monduli ambayo husaidia wanyama kwenda hifadhi ya tarangire na hifadhi ya Manyara.
Mtafiti wa wanyamapori katika mradi wa Simba Tarangire, Dk Bernard Kissui alitoa taarifa hizo juz katika kikao cha kujadili kuokoa eneo la mapito ya wanyama kwa kuchinja hadi Mdori ambalo linaendelea kuvamiwa .

Dk Kissui alisema kati ya januari hadi Desemba 2019, wamebaini wanyama 380kugongwa katika barabara hiyo hali ambayo inatishia uhai wa hifadhi za taifa zaTarangire na Alisema
katika eneo hilo ,licha ya wanyama kugongwa pia kuna uvamizi mkubwa wa
wananchi, kulima na kuweka makazi ndani ya eneo hilo. “Kama
serikali isipochukuwa hatua sasa, wanyama wengi watapotea lakini pia tutaathiri
ikolojia ya Tarangire na Manyara”alisema

Alisema wanyama hao, wanagongwa wengi nyakati za
usiku hasa kutokana na mwendokasi ya magari.

NaibuWaziri wa Maliasili na Utalii, Costantite Kanyasu, aliagiza Shirika la hifadhi
za Taifa(TANAPA), kwa kushirikiana na Mamlaka ya Wanyamapori(TAWA) na Taasisi
ya Utafiti wanyamapori(TAWIRI), kuandaa mabango na kuweka katika eneo la
barabara hiyo kutoka Arusha hadi Babati.


“naagiza kuwekwa mabango ya kuonesha faini ukigonga mnyama mfano simba dola 4000, pia yawekwe mabango ya kupunguza mwendo kwa kuonesha wanyama wanaovuka maeneo hayo" alisema.

Alisema pia atazungumza na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi,ili kuhakikisha zinawekwa alama za kupunguza mwendo za kisasa ambazo haziwezi kuisha kwa muda mfupi.

Mkurugenzi wa utafiti wa TAWIRI, Dk Julius Keyyu alisema ili kuokoa wanyama na mapito yao ni muhimu kuwepo ushirikiano baina ya wananchi, viongozi wa vijiji na wadau wa
utalii.

Dk. Keyyu alisema tayari taasisi kadhaa zimekuwa zikifadhili mradi wa kufatilia
wanyama, ikiwepo taasisi ya Chemchem Foundation ambayo imegharamia mradi wa Tembo katika eneo hilo kufungwa vifaa vya mawasiliano kufatilia mapito yao.

Mkurugenzi wa Wanyamapori nchini, Dr Maurus Msuha alisema ni lazima sasa serikali kwa kushirikiana na wadau kuchukuwa hatua za kulinda eneo hilo la mapito ya wanyama alisema

Katika kulinda eneo hili ni lazima barabara kuwekwa alama na kutolewa adhabu kwa wanaogonga wanyama lakini pia katika kulinda mapito ya wanyama wananchi wanapaswa kushirikishwa ili kupisha maeneo ya mapito ya wanyama
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad