5/25/2020

Whozu Amfunga Kengele MremboTunda, Habanduki Uslay Qeen Wote Kwishney


ANASTAZIA Sebastian Kimaro almaarufu kama Tunda, ni mwanadada mrembo ambaye amekuwa akitambulika kama muuza nyago ‘video vixen’ kwenye video za nyimbo za wasanii wa Bongo Fleva.

Tunda ameonekana kwenye video kama Augelina, Sina Makosa, Raha, Salome ya Diamond Platnumz, Nimefurahi ya Young D, Doko ya Whozu na nyinginezo.

Mrembo huyu amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume tofautitofauti, kabla ya jahazi lake kutia nanga kwenye penzi zito la mwanamuziki wa Bongo Fleva, Oscar Lelo ‘Whozu’ ambaye amefanikiwa kumfunga breki.

Makala haya yanakuletea baadhi ya wanaume waliowahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Tunda kabla ya kunasa kwa Whozu;

STAN BAKORA

Stanley Yusuph ‘Stan Bakora’, ni msanii wa vichekesho na filamu Bongo. Amewahi kusikika akisema kuwa Tunda alikuwa ni mpenzi wake wa kitambo tangu wakiwa Morogoro, Mwaka 2012 kabla ya kupotezana. Baadaye walikuja kukutana jijini Dar na kuendeleza penzi lao japokuwa halikudumu.

YOUNG D

David Genzi ‘Young D’ ni staa wa Bongo Fleva. Yeye ndiye alitabiriwa kuwa lazima asogeze jiko ndani. Tunda na Young D walipendezana kinoma, kiasi kwamba hakuna ambaye aliwaza kuwa wangekuja kuachana, maana hata mrembo huyo alitumika kama video vixen katika ngoma ya Young D ya Nimefurahi. Sababu ya kuachana kwao ni baada ya Tunda kuonekana kama hajatulia na baadaye kila mmoja kushika hamsini zake.


JANJARO

Mwanamuziki mwingine wa Bongo Fleva, Abdul Chande almaarufu Dogo Janja au Janjaro, naye anasemekana kuonja tunda la Tunda japokuwa penzi lao lilikuwa la kimyakimya na halikudumu kwa muda mrefu.

NUH MZIWANDA

Kuna wakati Tunda alionekana kwenye mahaba na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’. Hii ilikuwa baada ya kuvuja kwa picha zao za kimahaba mitandaoni, lakini hakuna kati yao aliyekubali kuwa wanatoka.

DIAMOND PLATNUMZ

Baada ya mrembo huyu kushiriki katika video ya Ngoma ya Salome ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kama video vixen mwaka 2016. Baadaye zilianza kusikika tetesi kuwa wanatoka kimapenzi japo wote wawili walikuwa wakikanusha. Ukweli ulikuja kufichuka baada ya video call yao kuvuja kabla ya Tunda kunaswa nyumbani kwa jamaa huyo, enzi zile anaishi Madale.

CASTO DICKSON

Aliyekuwa mtangazaji wa Clouds TV, Casto alizama kwenye penzi la Tunda kiasi kwamba akachora tatuu yenye jina la mrembo huyo. Baadaye walibwagana bila kujulikana sababu ya msingi.

ALI

Tunda, baada ya kubwagana na Casto, habari zikasambaa mjini kuwa anatoka na jamaa fulani hivi aliyejulikana kwa jina la Ali.

Tunda hakutaka kumweka hadharani watu wamjue kwa sababu ni mtu mstaarabu, mwenye pesa zake, ambaye hapendi kujiweka mitandaoni. Penzi lao liliyumba baada ya Tunda kuanza kutoka na Whozu.

WHOZU

Whozu ni mchekeshaji na mwanamuziki wa Bongo Fleva. Kwa sasa ndiye amefunga listi ya wanaume waliotembea na Tunda. Wawili hawa walianza uhusiano kimyakimya kabla ya kujulikana hadharani. Tunda aliwahi kusema kuwa yeye na Whozu hawajajuana leo wala jana, bali wamejuana kitambo wakiwa washkaji, wamesoma shule moja kule Moshi. Whozu anajulikana hadi kwa wazazi wa Tunda.

Tunda aliwahi kushiriki katika video ya Wimbo wa Whozu wa Doko akiwa video vixen kama alivyofanya kwa Young D na Diamond.

Ilikuwa ni ngumu watu kuamini kwani Tunda alizoeleka kama mwanamke wa kubadili sana uhusiano na wanaume tofautitofauti, lakini kwa sasa ametulia na bwana mdogo huyo ambaye inasemekana wapo njiani kufunga pingu za maisha.

MAKALA: HAPPYNESS MASUNGA, BONGO
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger