5/26/2020

Zari Atakubali Kuolewa Mke wa Pili au wa Tatu?
UNAWEZA kusema mwanamama mjasiriamali wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, raia wa Uganda mwenye maskani yake pale Durban nchini Afrika Kusini, hana bahati ya mapenzi. Nitajenga hoja!

 

Hata hivyo, huu ni uthibitisho kwamba, huwa anafanya uamuzi mbaya linapokuja suala la kuingia kwenye mapenzi, ndiyo maana inaaminika hana bahati na mapenzi.

Vyovyote itakavyokuwa, lakini Zari ana stori ndefu kwenye mapenzi ambayo kwa bahati mbaya, si stori nzuri kwa sababu mahusiano yake mengi hayakudumu.

 

Mpenzi wa kwanza wa Zari aliyefahamika kwenye umma, alikuwa ni jamaa mmoja aitwaye Rasta Rob, raia wa Uganda.

Huyu jamaa stori yao haikuishia vizuri kwani aliishia kumpiga Zari picha chafu na kuzisambaza, hivyo kumharibia sivii yake kwenye jamii.

 

Baada ya hapo, walipitapita vijana wengine, lakini hawakuwa ofisho hadi alipofika mtu mzima, marehemu Ivan Ssemwanga, Don mwenyewe ambaye alimuoa na kuzaa naye watoto watatu wa kiume; Pinto, Raphael na Quincy ambao ni chapa kamili ya jamaa huyo kutokana na walivyofanana naye.

 

Hata hivyo, wakati Zari anashindwana na Ivan, alimtuhumu kuwa alikuwa ni mwanaume katili sana kwake.

Tuhuma hizi dhidi ya mumewe huyo, Zari alizitoa wakati akiwa kifuani mwa mwanaume mwingine Simba aliyemrithi Ivan ambaye ni mwanamuziki mkubwa barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

 

Sote tunajua ni kwa jinsi gani uhusiano wa Zari na Mondi ulivyokuwa na drama nyingi. Kulikuwa na milima na mabonde ya kutosha.

Wakiwa pamoja, walijaaliwa watoto wawili; Tiffah Dangote na Prince Nillan.

Pia sote tunajua uhusiano wa wawili hawa uliishia pale Zari alipoposti uaridi jeusi. Hiyo ilikuwa ni valentine’s Day, Februari 14, 2018.

 

Vyovyote itakavyokuwa, hayo ndiyo mahusiano maarufu zaidi ya Zari ndani na nje ya Afrika Mashariki. Kidogo uhusiano mwingine uliosikika kihivyo ni ule wa King Bae ambaye aligoma kumfunua uso akiogopa nyakunyaku kumnyakua.

Zari alidai kufunga ndoa ya kiserikali na King Bae kule Afrika Kusini huku akimtumia jamaa huyo kueleza madhaifu ya Diamond ambapo alisema jamaa huyo alikuwa anajua kuziba gepu lake kwa ufanisi mkubwa mno.

 

Ghafla tu, King Bae akapotea. Zari akamsahau. Kuna wakati aliulizwa juu ya jambo hilo, akadai kuwa jamaa huyo ‘alikufa’.

Baada ya hapo, Zari alionekana mitandaoni na ‘kitoto’ kinachochipukia kwenye muziki nchini Uganda.

Watabiri wa mambo wanasema hata huo uhusiano wake na hicho kibenteni, hauwezi kudumu hata kama Zari ana umri wa miaka 30, ongezea na watoto watano, hawezi kuwa chini ya mtoto mwenye umri wa miaka 18!

 

Hapa ndipo tunapohitimisha makala hii kwa kusema kuwa, njia pekee ya Zari mwenye umri wa miaka 40 kuingia kwenye ndoa kwa mara nyingine ni kukubali kuwa mke wa pili au watatu. Huyo ndiye mwanaume pekee atakayemfaa Zari.

Yawezekana ikawa ni ngumu zaidi kumpata kijana wa kumuoa ambaye ni freshi kwa maana hajaoa au kutalikiana na wenza wake.

 

Ukweli unabaki kuwa, mwanaume mwenye viwango vyake, hawezi kumfungulia milango ya nyumbani kwake na moyo wake kwa mwanamke kama yeye ambaye rekodi zake za kudumu na mwanaume zinamhukumu.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger