Zitto Kabwe kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kutoa matamshi ya uchochezi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Kiongozi wa chama cha upinzani ACT-Wazalendo nchini Tanzania ametiwa hatiani na mahakama jijini Dar es Salaam na kuhukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja kwa sharti la kutotoa kauli za kichochezi. 

Chama chake cha ACT tayari kimetoa taarifa ya kuwa bwana Kabwe anapanga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo. 

Mahakama hiyo imemtia hatiani Zitto kwa makosa yote matatu ya uchocheji yaliyokuwa yanamkabili. 

Hukumu hiyo iliyotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi imekuja baada ya kipindi cha zaidi ya mwaka mzima wa kesi kuunguruma, kwa mara ya kwanza bwana Zitto kufikishwa mahakamani kusikiliza kesi zake ilikuwa Novemba 2, mwaka 2018.

Zitto anadaiwa kutenda makosa hayo ya uchochezi Oktoba 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari. 

Chama cha ACT kupitia makamu mwenyekiti wake Dorothy Semu kimetoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa hukumu dhidi ya kiongozi wao haikubaliki na wataipinga mahakamani. 

"Hukumu hii ni sawa na kumzuia Zitto kusema chochote cha kuikosoa serikali na rais katika mwaka wa uchaguzi," inaeleza sehemu ya taarifa ya Bi Semu. 

"Hukumu hii haiwezi kukubalika. Inaweza kuwa mfano wa kuminya uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza Tanzania."

Bi Semu ameituhumu serikali ya chama tawala nchini Tanzania CCM kwa kile alichokiita "kutumia mashtaka ya uchochezi kuwanyamazisha wale wanaongea ukweli dhidi ya serikali.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jamuhuri, Adhabu aliyopewa kulingana na kosa Jmuhuri sisi Watanzania hatujatendewa haki kwa hiyo Ni vyema tukatiwe Rufaa juma tatu ili apewe Adhabu kali Zaidi iiwemo kwenda Lupango mvua isizo pungua 15.

    Hivi sasa yuko na genge lake teule Katika Mahospitali Amana/ Mloganzila/ M.nyamala anatafuta Data za waathirika ili apotoshena kuchochea kwa baadhi ya Balozi hapa nchini. na zinine katika magazetiya huko Australia (Sydney harald).

    Uchochezihuyu Dogo ni Hulka yake naAina shakka.

    Jamuhuri mjipange ki sawa sawa.
    Jumanne na Nassoro jalada mnalo lifanyieni kazi stahiki. Biswalo fatilia ipasavyo. Kumyamazisha ni Bora
    na itapendeza akihifadhiwa vile vile.

    ReplyDelete
  2. Jamuhuri, Adhabu aliyopewa kulingana na kosa Jmuhuri sisi Watanzania hatujatendewa haki kwa hiyo Ni vyema tukatiwe Rufaa juma tatu ili apewe Adhabu kali Zaidi iiwemo kwenda Lupango mvua isizo pungua 15.

    Hivi sasa yuko na genge lake teule Katika Mahospitali Amana/ Mloganzila/ M.nyamala anatafuta Data za waathirika ili apotoshena kuchochea kwa baadhi ya Balozi hapa nchini. na zinine katika magazetiya huko Australia (Sydney harald).

    Uchochezihuyu Dogo ni Hulka yake naAina shakka.

    Jamuhuri mjipange ki sawa sawa.
    Jumanne na Nassoro jalada mnalo lifanyieni kazi stahiki. Biswalo fatilia ipasavyo. Kumyamazisha ni Bora
    na itapendeza akihifadhiwa vile vile.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau, Umesha sikia.!
      DOMO LA CHOO..??

      Basi huyu Dogo ni HULKA YAKE.

      Hata umpe masaa 72 hawezi bila
      kupotosha ataumwa na kwenda zahanatiyake Mabibo.

      Tunoba Jamuhuriiliimamiie hili
      ipasavyo na Adhabu kali zaidi ya
      kuwa fundisho kwa wenyenia ovu kama huyu na kma hawa wanao jipongeza "Umeona yangu mpya mtandaoni"

      Ni lazima wakomeshe na wapate fundisho.

      Delete
    2. Mdau, Umesha sikia.!
      DOMO LA CHOO..??

      Basi huyu Dogo ni HULKA YAKE.

      Hata umpe masaa 72 hawezi kukaa bila
      kupotosha,anawashwa na ataumwa na kwenda zahanati yake Mabibo.

      Tunataka Jamuhuri ilisimamie hili
      ipasavyo na Adhabu kali zaidi itolewe ya kuwa fundisho kwa wenye nia ovu kama huyu, na kama hawa, wanao jipongeza "Umeona yangu mpya mtandaoni

      Ni lazima wakomeshe na wapate fundisho.

      Delete

Top Post Ad