Juma Jux "Huddah Ana Vigezo Ninavyohitaji Kwa Mwanamke Kuwa Mpenzi Wangu"BAADAya maneno kuwa mengi mtandaoni kuwa staa wa Bongo Fleva, Juma Mussa ‘Jux’ ana uhusiano wa kimapenzi na mrembo wa Kenya, Huddah Manroe ‘Huddah’ hatimaye mkali huyo wa RnB amefunguka kuwa habari hizo sio za kweli licha ya kuwa bidada huyo ana vigezo vyote anavyovihitaji.

Akizungumza na Mikito Nusunusu, msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Covid-19, alisema kwamba ameona watu wanavyosema mitandaoni kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mrembo huyo, jambo ambalo halina ukweli kwa sababu tayari msichana huyo ana mtu wake.

“Ni msichana mrembo, ana asilimia kama themanini hivi ya vigezo ninavyovihitaji kwa mwanamke, lakini hiyo haifanyi mimi na yeye tukawa wapenzi, namheshimu kama dada yangu na tumekuwa tukishirikiana sana kwenye kazi, isitoshe Hudah ana mtu wake,” alisema Jux.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE