6/19/2020

Kauli ya Katambi Kuhusu Kuoa...Afikiria Kurudiana na Fatma Karume Sababu Anagombea UraisMkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi amesema kuwa lazima atatekeleza agizo alilopewa na Rais Magufuli haraka iwezekanavyo, lakini hawezi kurudiana na 'Ex' zake alioachana nao.


Kauli hiyo ameitoa leo Juni 18, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kusema kuwa upendo aliooneshwa na Rais Magufuli ni mkubwa hivyo hawezi kumuangusha, na kwamba anajipanga ili akutane na mke sahihi.

"Wachumba niliokuwa nao ni hao wawili kwa nyakati tofauti, sasa hivi tena inabidi nikae nijipange lakini agizo la Rais Magufuli nitalitekeleza haraka iwezekanavyo, ila nadhani tunaweza tukarejeana na Fatma Karume kwa sababu nasikia anataka kugombea Urais kupitia chama kile, pengine nikawa mume wa mgombe Urais" amesema DC Katambi.

Siku za hivi karibu Rais Magufuli aliwaagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi, waoe haraka kwa kuwa wanawake wazuri ni wengi na kwamba Jiji kama hilo haliwezi kuongozwa na watu ambao hawajaoa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

2 comments:

 1. Itapendeza, Shangazi anahitaji penzi,
  alinilalamikia sana. Mradi umetoa Ofa
  na Mimi natoa Ofa kwa Halima. jibu withhin 21 Days from today.

  St Gasper nimesha wataarifu Nia zetu
  kukodisha Hall kwa Tafrija hii. Tarehe
  itapangwa baada ya makubaliano ya pande zote husika. MCHAKATO UNAENDELEA

  ReplyDelete
 2. Itapendeza, Shangazi anahitaji penzi,
  alinilalamikia sana. Mradi umetoa Ofa
  na Mimi natoa Ofa kwa Halima. jibu withhin 21 Days from today.

  St Gasper nimesha wataarifu Nia zetu
  kukodisha Hall kwa Tafrija hii. Tarehe
  itapangwa baada ya makubaliano ya pande zote husika. MCHAKATO UNAENDELEA

  ReplyDelete

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger