6/22/2020

Kim Kardashian Alamba Dili la Mamilioni SpotifyMwanama Kim Kardashian ameripotiwa kuingia mkataba na mtandao wa Spotify kwaajili ya kutengeneza na kutangaza kipindi kipya (Podcast) ambayo itajikita kwenye masuala ya kesi za watu waliohukumiwa kimakosa na harakati za kushinikiza mabadiliko ya sheria za haki za kijinsia.

Dili hilo limekuja baada ya Spotify kuamua kujikita kwenye vipindi vya mtandaoni (Podcast) ambapo mwaka jana walinunua podcast kubwa tatu kutoka kwa makampuni mbalimbali.

Bado haijawekwa wazi ni dili la shilingi ngapi lakini taarifa zinasema kuwa huenda ni pesa ndefu kwa sababu dili la mwisho lililofanywa na kampuni ya #Spotify kuhusiana na podcast liliigharimu kampuni hiyo dola za Marekani milioni 100.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger